Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 4 October 2014

WANAUME 400,000 WAFANYIWA TOHARA


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.

Na Moshi Lusonzo
Serikali imesema jumla ya wanaume 400,000 kutoka mikoa minne nchini, wamefanyiwa tohara katika kampeni iliyomalizika hivi karibuni.

Katika hotuba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii, Dk, Seif Tashid,  iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Michael, wakati wa ufungaji wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam jana, alisema  mikoa iliyohusika na kampeni hiyo ni Iringa, Njombe na Tabora.



Zoezi la kuwafanyia tohara wanaume lililofahamika kama `tohara ya kitabibu ya wanaume’ (VMMC) iliendeshwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania, Marekani na Shirika la Jhpiego.

Alisema  zoezi hilo limesaidia kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vinavyosababisha Ukimwi (VVU) nchini, kitu kinachoonyesha lengo la kufikia maambukizi ya asilimia 0.16 hadi mwaka 2018 linaweza kufikiwa.

Baada ya kuonekana kwa mafanikio hayo, mikoa mingine 12 ambayo wanaume wake wapo nyuma katika kufanyiwa tohara imeteuliwa kuendelea na zoezi hilo.
Kiasi cha Dola za Marekani Milioni 34 zimetengwa kwa ajili ya kuendesha kampeni hiyo.

Dk. Rashid alisema lengo ni kuwafikia watu milioni 2.1 walio na umri kati ya miaka 10 hadi 34 kufikia mwaka 2017.

Awali, Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini (USAID), Timoth Donny, alisema katika tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba wanaume waliofanyiwa tohara wanaondokana na hatari ya kuambukizwa VVU kwa silimia 60, hivyo kuna wajibu wa kuhakikisha elimu inatolewa sehemu zote nchini.

Alisema nchi yake ipo tayari kusaidia katika kupambana na hali hiyo katika nyanja ya kujengea uwezo wa mafunzo na vitendea kazi kwa watoaji huduma.

Naibu Rais wa Shirika la Jhpiego, Alain Damiba, pamoja na kuishukuru serikali kwa kutoa msaada mkubwa katika kutekeleza mkakati huo, shirika lake kwa kushirikiana na washirika mbalimbali litaendelea kufanya kazi kwa ajili ya kuboresha afya za wananchi na kuongeza kasi ya maendeleo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment