Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 5 January 2014

UKWELI WA KIFO CHA MGIMWA, KIGHOMA MALIMA, HORACE KOLIMBA, STEVEN KIBONA NA GILMAN RUTIHINDA

Mgimwa
Profesa Kighoma Malima
Gilman Rutihinda

Ndugu zangu,
Watanzania wanajiandaa kumzika aliyekuwa Waziri wa Fedha (Mweka Hazina Mkuu wa Serikali) marehemu William Mgimwa, maziko ambayo yatafanyika Jumatatu kijijini kwao Magunga, mkoani Iringa.

Kumekuwepo na tetesi nyingi kupitia vyombo vya habari kwamba huenda waziri huyo mkimya amelishwa sumu. Hakuna aliyethibitisha madai haya tangu kutokea kifo hicho Januari Mosi 2014.
Kifo cha Mgimwa kimeingia kwenye mlolongo wa vifo kadhaa vyenye utata vilivyowahi kutokea nchini katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Mawaziri wawili waliopata kuongoza Wizara ya Fedha nao wanadaiwa kufa katika mazingira ya kutatanisha, miongoni mwao akiwa Profesa Kighoma Ally Malima aliyekufa Julai 16, 1995.
Alipojiengua CCM na kuhamia NAREA (NRA), Prof Kighoma alikwenda Makka katika hijja ya UMRA. Kabla ya kwenda kwake huko aliahidi pindi atakaporudi Tanzania atakuja kutoa yaliyopo moyoni mwake. Baada ya kumaliza hijja alielekea Uingereza na mauti yakamkuta huko.
Ilienea katika kila kona ya Tanzania kuwa inawezekana kuna FITNA iliyosababisha kifo chake japokuwa wengine wanasema hakuna FITNA yoyote. 

Steven Kibona, aliyepata kuwa Waziri wa Fedha enzi za Alhaj Ali Hassan Mwinyi, pamoja na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Gilman Rutihinda, nao walikufa vifo vya utata.
Kuna taarifa zilizodai kwamba, wazalendo hao walikataa kuchapisha fedha na kuziingiza kwenye mfumo kwa kutambua kwamba kufanya hivyo kungeongeza mfumuko wa bei na ugumu wa maisha ungeongezeka.
Kibona alipelekwa na aliporejea huko akaanza kuumwa. Ikaelezwa kwamba amekula vyakula vya Kihindi ndiyo maana alikumbwa na tumbo la kuhara kwa sababu ya ugeni wa chakula. Hakukaa muda mrefu akafariki dunia.
Rutihinda naye alipata ajali asubuhi tu akiwa anatoka nyumbani kwake. Taarifa zilizokuwepo ni kwamba ilikuwa ajali ya kawaida!
Mwingine ambaye kifo chake kina utata ni Horace Kolimba. Huyu anajulikana kwa kauli yake aliyoitoa kwamba CCM haikuwa na dira wala mwelekeo. Akaitwa Dodoma 'kuhojiwa'. Lakini Machi 15, 1997 majira ya saa 11 jioni wakati akijiandaa kutoa maelezo yake, akadondoka ghafla. Walipompeleka hospitali ya Mkoa wa Dodoma tayari alikuwa 'wa jana'.
Hivi, hakuna anayeweza kutoa taarifa rasmi kuhusiana na vifo hivi vyenye utata au kifo cha kiongozi yeyote kinapotokea mpaka tusubiri 'redio mbao'?
Nawasilisha.

No comments:

Post a Comment