Hii ni jezi mpya ya Arsenal? Thierry Henry akiwa na Bacary Sagna, Linford Christie na Olivier Giroud
KLABU ya Arsenal imetangaza kuingia Mkataba wa muda mrefu wa udhamini wa vifaa vya michezo na kampuni ya Puma kuanzia Julai mwaka 2014.
Pamoja
na hayo hakuna kiwango cha fedha cha udhamini huo kilichothibitishwa
Jumatatu, ingawa dili hilo linatajwa kama kubwa zaidi katika historia ya
uhusiani wa Puma na Arsenal.
Inafahima
Washika Bunduki hao wanapokea kiasi cha Pauni Milioni 30 kwa mwaka
kutoka kwa wadhamini wakuu, shirika la ndege la Emirates, na imeripotiwa
dili hilo jipya litakuwa sawa na lile ambalo Puma walitoa wakati
wanaiponya timu hiyo Nike, waliokuwa wadhamini wa Arsenal tangu 1994.

Hii iko hivi! Picha ya jezi mpya ya Arsenal, ambayo ni sawa na ile aliyokuwa anavaa Henry, imevuja kwenye Twitter

Mtendaji Mkuu, Ivan Gazidis (kulia) akipeana mikono na Mtendaji Mkuu wa Puma, Bjoern Gulden

Dili imetiki: The Gunners imetangaza kuingia Mkataba wa muda mrefu na Puma katika Mkutano na Waandishi wa Habari Jumatatu.
<BIN ZUBEIRY>
No comments:
Post a Comment