Na Bety Joseph, Arusha
MKUU wa Wilaya ya Arumeru, Munasa Nyirembe amewataka madiwani katika Halmashauri ya Arusha Vijijini kuhakikisha kuwa wanakuwa wakulima na wafugaji wazuri ili waweze kuwa mfano wa kuigwa na jamii .
Hata hivyo, mbali na kuwa na mashamba lakini pia hata mifugo ya kufuga pia wanatakiwa kuunga mkono kauli ya kilimo kwanza kwa matendo na wala sio maneno kama ilivyozoeleka kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa.
Alisema kuwa kudai na kusisitiza matumizi ya Kilimo kwanza pekee kwa njia ya mdomo bado hayatoshi kwani kwa sasa kinachohitajika zaidi ni vitendo na wala sio maneno ambayo wakati mwingine hayatekelezwi.
Aliendelea kwa kusema kuwa ili kuweza kuunga mkono kauli hiyo ya Kilimo kwanza ni lazima hata viongozi wenyewe wahakikishe kuwa wanaaanzan kulima lakini hata kufuga kama mfano ikiwa ni jitiaada zaidi za kuongeza na kuimarisha kilimo kwanza.
"Inasikitisha sana kama sisi Madiwani hata wakuu wa wilaya tutasimama na kudai kuwa kilimo kwanza kinatakiwa kutekelezwa kwenye maeneo yetu alafu sisi hatuna hata shamba moja la mfano itakuwa ni aibu tupu ni lazima sasa tuanze kulima 'aliongeza zaidi Munasa.
Pia alidai kuwa kama madiwani wa Halmashauri hiyo ya Arusha Vijijini watawea kuweka utaratibu huo wa kulima basi itaweza kuwa kazi raisi sana ya kuweza kusisitiza kilimo kwanza kwani wananchi wataona umuhimu wa kulima lakini kufuga kwa kutumia mbinu za kisasa zaidi.
"Unapokuwa na shamba au unapofuga alafu ukamuambia mwananchi kuwa kilimo kwanza ni dili basi anaweza kuiga lakini diwani mzima huna shamba wala ufugi chochote sasa huyo mwananchi ataiga nini kizuri toka kwako ni lazima sasa tubadilike"aliongeza Munasa.
Alimalizia kwa kusema kuwa ili kilimo kwanza kiweze kuendelea ni lazima kuwepo na ushahidi kuanzia kwa viongozi wa aina zote lakini pia kuwepo na moyo wa uzalendo ambao utalenga kufanikisha zaidi sera za kilimo kwanza.
No comments:
Post a Comment