Naibu
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt Mahongoro Mahanga
akitoka katika chumba cha mahakama ya kazi, Tume ya Usuluhishi na
Upatanishi wiki iliyopita siku ya Jumanne baada ya kusomewa mashtaka
yake ya kumfanyisha kazi PS wake (Private Secretary) Bi, Itika Kasambala
katika ofisi yake ya Bunge kwa muda wa miaka kumi bila mkataba na
kusitisha kazi yake na kisha kulipa mafao ya laki mbili tu.
Naibu
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana akishuka katika kazi za
mahakama ya kazi, Tume ya Usuluhishi na Upatanishi wiki iliyopita siku
ya Jumanne jijini Dar es Salaam.
Bi. Itika Kasambala akiwa katika moja ya vyumba vya habari baada ya kufanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi.
Baadhi ya nakala za malada ya kesi hiyo iliyofunguliwa mahakama ya kazi, Tume ya Usuluhishi na Upatanishi na Bi. Itika Kasambala dhidi ya Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana.
.Baada ya miaka kumi amlipa mafao ya laki mbili tu.
.Dada alalama kwamba Naibu Waziri alimtaka kimapenzi akakataa
Na. Mwandishi wetu
NAIBU Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt Makongoro Mahanga ameingia kwenye kashfa nzito ya kuvunja sheria za kazi nchini kwa kumfanyisha kazi msaidizi wake (PS) wa ofisi yake Bunge kwa miaka kumi bila mkataba na kumlipa fedha taslimu shilingi laki mbili tu (200,000) kama mafao.
Naibu Waziri, Mahanga anakuwa kiongozi wa kwanza kuingia kwenye kashfa akiwa madarakani tena kwenye swala la ajira wakati yeye mwenyewe ni waziri mwenye dhamana na maswala ya ajira na haki za wafanyakazi nchini chanzo chetu kimeelezwa.
Kwa mujibu wa sheria kazi na mahusiano kazini, Naibu Waziri amekiuka kifungu cha 3 cha sheria ya Taasisi za kazi za mwaka 2004 na pia amekiuka sehemu ya tatu ya viwango vya ajira na sehemu ndogo A kwa kushidwa kuandika mkataba kwa mujibu wa kifungu cha 14 ibara ya kwanza kama sheria ya kazi na mahusiano kazini inavyotaka.
Katika kifungu hicho cha 14 ibara ya kwanza kinasema mkataba utakuwa wa kipindi cha muda usiotajwa, mkataba wa kazi maalumu na mkataba unatakiwa kuwa wa maandishi ambapo vyote Mhe Naibu Waziri hakufanya.
Ibara ya 15 kifungu cha.-(1) kinasema kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (2) cha kifungu cha 19, mwajiri anatakiwa kumpa mfanyakazi, wakati mfanyakazi anapoanza kazi, taarifa zifuatazo kwa maandishi, jina, umri, anuani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi; mahali alipoajiriwa; kazi zake; tarehe ya kuanza; muundo na muda wa mkataba; kituo cha kazi; masaa ya kazi; ujira na njia ya ukokotoaji wake, na taarifa za mafao mengine.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Bi. Itika Kasambala (31) anasema alianza kazi kwa Mbunge huyo wa Segerea na Naibu Waziri wa kazi Dkt. Mahanga, mwaka 2003 kama PS (Personal Secretary) kwa makubaliano ya kumpa mshahara wa shilingi 120,000 kwa mwezi lakini alianza kumlipa shilingi 50,000 tu.
“aliniambia kwamba nianze kazi kwanza baadaye atanipa mkataba wa ajira na kunilipa mafao ya hifadhi ya jamii na matibabu lakini baada ya miaka kumi ananitumia sms akiwa Dodoma kwamba kazi basi sikuhitaji tena,” Kasambala alisema.
Amesema kwamba Mbunge huyo alimtumia sms akiwa kwenye vikao vya bunge mjini dodoma mwaka jana mwezi wa sita akimjulisha kwamba ajira yake imeshafika kikomo kwa sababu hana uwezo tena wa kumlipa mshahara na mahitaji mengine ya kiofisi.
Kasambala aliendelea kusema kwamba mara ya kwanza wakati anaanza kazi mwezi wa tano mwaka 2003 baada ya msaidizi wa ofisi ya mbunge Mahanga kuacha kazi na ndipo alipotafutwa yeye na walikwenda kuelewana kwa malipo ya 120,000 kwa mwezi.
Alisisitiza kwamba mara baada ya kuanza kazi kwa ofisi ya mbunge alikuwa analipa pesa kupitia mkononi na baadaye tigo pesa na baada ya muda akawa anachukua pesa yake ya mshahara toka katika manisapaa ya Ilala kama posho ya Mhe Mahanga kama diwani kila mwezi.
Dada huyo kwa mshangao baada ya mahojiano ya muda mrefu alikiri kwamba Mhe Mahanga alikuwa na nia ya dhati kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na kumtaka aende Dodoma lakini alikataa kufanya masharti hayo.
“mwaka juzi baada ya kuonyesha nia ya kunitaka kimapenzi alinipigia simu akitaka niende Dodoma bungeni kwa mazungumzo zaidi kama msaidizi wake lakini nilikataa,’ aliongeza Kasambala.
Amesema tangu aanze kazi kwa Mhe Mahanga hakuwa anatoa huduma zozote kama matibabu au fedha kwa ajili ya sikukuu ilikuwa ni mshahara tu wa 120,000 kwa mwezi lakini kila akimfuata ili waandikishiane mkataba alikuwa akizungumsha bila sababu za msingi.
Bi. Kasambala aliongeza kuwa amefanya kazi Mhe Mahanga tangu akiwa mbunge wa Ukonga na baadaye Segerea lakini ameshidwa kuheshimu sheria za ajira na taratibu za kazi wakati yeye mwenyewe ni waziri mwenye dhamana ya ajira kwa watanzania.
Amesema mwaka jana tarehe 14/09/2013 alimtumia kwa Tigopesa kiasi cha shilingi za Tanzania 200,000 kama mafao yake baada ya kufanya kazi kwa takribani miaka 10 kama Msaidizi wake wa Ofisi ya Mbunge.
Amesema kwamba aliamua kwenda Chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi, Mahoteli, Majumbani na Kazi Nyingine (CHODAWU) kwa msaada wa ksiheria ba baada ya kukutanishwa bado Mhe Mahanga akawa mgumu kukubaliana kiungwana mpaka ikawalazimu kwenda mahakani Tume ya Usuluhishi na Upatanishi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi wakili wa Kasambala, Nyaisa Godwin alisema kuwa kesi imefunguliwa mahakama ya kazi wiki iliyopita siku ya Jumanne, Tume ya Usuluhishi na Upatanishi kesi namba CMA/DSM/ILA/R.711/13.
Wakili Nyaisa alisisitiza kwamba Naibu Waziri aliiambia mahakama kwamba Dada Kasambala alikuja kufanya kazi kwake kama mwanafunzi wa chuo kwenye mazoezi lakini alishidwa kuithibitishia mahakama kwa ushawishi wa barua ya (field to chuoni).
“tulishagazwa na majibu ya waziri kwamba dada huyo alikuwa field, na nilimuuliza field ya miaka kumi? Alishidwa kutoa jibu mbele ya mpatanishi (Arbitrator),” amesema Nyaisa.
GPL
No comments:
Post a Comment