Ndugu zangu,
Hivi karibuni kulikuwa na Operesheni Tokomeza Ujangili ambayo ilisitishwa na serikali baada ya wabunge kueleza kwamba ilikiuka misingi ya haki za binadamu.
Hali hiyo ilisababisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, kujiuzulu huku mawaziri wengine watatu ajira zao zikitenguliwa.
Uamuzi wa kuanzisha operesheni hiyo ulitokana na wimbi la ujangili ambalo limemaliza tembo katika hifadhi zetu huku madai yaliyokuwepo yakisema ujangili unahusisha vigogo wengi.
Wakati wa operesheni hiyo, Mbunge wa Tunduru, Mtutura Abdallah Mtuturu, anadaiwa kuhojiwa na 'kamati' hiyo ya operesheni tokomeza kuhusiana na tuhuma mbalimbali za ujangili zilizotolewa dhidi yake hata kabla ya kuanzishwa kwa operesheni hiyo.
Katika miaka ya nyuma, Mbunge
wa Songea Ali Yusuf Abdurabi alifungwa miaka 9 jela. Kosa
lilikuwa ni kukutwa na PEMBE ZA NDOVU zilizojaa kwenye Land Rover yake ya Ubunge. Na mfumo wetu wa ulinzi uliweza kubaini uhalifu huo huko huko Songea, leo mpaka Wachina
wanakamatwa na makontena ya meno ya tembo bandarini ina maana hakuna ajuaye?
Picha hii ni ya kwenye maktaba ya MJENGWA.
No comments:
Post a Comment