Na Mwandishi Wetu, Arusha
SERIKALI imeshauriwa kuhakikisha kuwa inaweka mtaala wa mabadiliko ya tabia ya nchi kuanzia ngazi ya shule za msingi ili kuweza kukabiliana na majanga mbalimbali ambayo yanaikumbaa nchi ya Tanzania lakini pia ulimwengu mzima kwa sasa.
Kauli hiyo imetolewa na Peter Mroso ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Green Social Education(GRESOE) kutoka katika Chuo Kikuu cha Mt Meru wakati akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa chuo hicho katika mdahalo wa wanafunzi wa vyuo vikuu Arusha uliofanyika chuoni hapo mapema jana.
Mroso alisema kuwa kwa sasa asilimia kubwa ya wasomi wanafanya kujisomea mambo mbalimbali ambayo yanahusu mabadliko tabia nchi ingawaje kwa sasa nchi inateketea kutokana na majanga hayo hivyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kuwepo na mitaala ambayo inahusu mabadiliko
tabia Nchi.
Aliendelea kwa kusema kuwa endapo kama mitaala ya Tanzania ingeweza kuwa na somo la mabadiliko ya tabia ya nchi basi hata wanafunzi wenyewe wangweza kuwa mabalozi wazuri sana wa masuala hayo ya mabadiliko tabia ya nchi.
Amebainisha kuwa njia hiyo ya kuongeza somo la mabadiliko ya tabia ya nchi litaweza kuifanya Tanzania kuepukana na majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuweza kurudisha hali kama ilivyokuwa hapo mwanzo
"Sisi wasomi wa vyuo vikuu mkoa wa Arusha tunashauri kuwa ni vema kwa sasa somo la mabadiliko tabia ya nchi likawa ni moja ya mitaala ya Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine tusiwe tunasikia tu kuwa kuna mabadiliko tabia nchi wakati hata jamii yenyewe haijui ni nini hasa," alibainisha hivyo Mroso.
Mbali na hayo alidai kuwa nayo serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa inaweka mikakati mbalimbali ya kuweza kuwasaidia wananchi wake kwani tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa asilimia kubwa ya wananchi bado hawajajua vema masuala ya mabadiliko tabia nchi
"kuna haja na umuhimu mkubwa kwa serikali kama itaweza kuwaelimisha watu juu ya hatua ambazo zinatakiwa kuchukuliwa kama njia mbadala za kukabiliana na mabadiliko tabia nchi ambapo njia kubwa ni kuwaelimisha wananchijuu ya kilimo cha utunzaji wa mazingira ambacho kitaweza kuwasaidia kuepukana na mabadiliko hayo ambayo yanasababisha madhara kwenye nchi ya tanzania'aliongeza Mroso
Alimalizia kwa kuwataka nao wasomi kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali kuweza kujiweka utaratibuw a kufanya midhalo lakini kuelimisha umma juu ya hatua ambazo zinaweza kutumika ili kupambana na mabadiliko tabia nchi ambayo wakati mwingine ndiyo chanzo cha umaskini hata kwenye vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini.
No comments:
Post a Comment