Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 12 January 2014

MAN CITY YAREJEA KILELENI, KAZI IPO ENGLAND

Kazi nzuri: Mshambuliaji wa Manchester City, Edin Dzeko (kulia) akimtungua kipa wa Newcastle, Tim Krul kuifungia bao la kwanza timu yake

MABAO ya Edin Dzeko na Alvaro Negredo yametosha kuipa ushindi wa 2-0 Manchester City dhidi ya Newcastle Uwanja wa St James Park na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu England.Nyota wa Bosnia alifunga bao la kwanza dakika ya nane akiunganisha krosi ya Aleksandar Kolarov kumtungua kipa Tim Krul.

Kikosi cha Alan Pardew kilidhani kimepata bao la kusawazisha baada ya shuti la mbali la Cheick Tiote kumpita kipa Joe Hart na kutinga nyavuni, lakini likakataliwa kwa sababu Yoan Gouffran alikuwa ameotea. 
Negredo akaifungia City bao la pili dakika za majeruhi. Ushindi huo unaifanya City irejee kileleni baada ya kutimiza pointi 47 kutokana na mechi 21, ikiishusha Chelsea yenye pointi 46 baada ya kucheza mechi 21 pia katika nafasi ya pili. Arsenal sasa ni ya tatu kwa pointi zake 45, ingawa imecheza mechi 20.  

Unstoppable: Krul (right) can do nothing to prevent Dzeko's strike flying into the top corner of his goal
Krul (kulia) hakuweza kuuzuia mchomo wa Dzeko
Deadly: Dzeko runs off to celebrate his early goal at St James' Park
Dzeko akikimbia kushangilia baada ya kufunga
Mobbed: The Bosnian striker is congratulated by his team-mates after finding the back of the net
Anapongezwa na wenzake

No comments:

Post a Comment