ASKARI wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), wamekamata shehena ya meno ya tembo ambapo hadi sasa thamani yake haijafahamika. Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Madeni Kipande alithibitisha kukamatwa kwa mzigo huo ambapo alisema kuwa kwa sasa hawezi kulizungumzia suala hilo ila wizara yenye thamana ndio ina wajibu wa kufanya hivyo.“Ndugu mwandishi ukweli ni kwamba mzigo huo upo, lakini siwezi kuzungumzia mnataka mnifukuzishe kazi, mpaka waziri mwenye dhamana au Katibu Mkuu wao ndio wanaweza kulizungumzia hili kwa undani lakini si mimi,” alisema Kipande.
Alisema pamoja na askari wa idara ya
wanyamapori kuwepo katika eneo hilo, lakini bado anayetakiwa
kulizungumzia suala hilo ni mhusika mwenye dhamana na si vinginevyo.
Hivi karibuni shehena kubwa ya meno ya tembo ilikamatwa ikiwa na vipande 1,021 na uzito wa kilo 2,915 ambayo haijawahi kukamatwa nchini.
Kazi hiyo ya ukamataji wa meno hayo iliongozwa na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki katika Bandari ya Zanzibar.
CHANZO: Mtanzania

No comments:
Post a Comment