Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa
PPF Bi. Lulu Mengele akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu
maazimo yaliyofikiwa kwenye mkutano wa 23 wa wanachama na wadau wa mfuko huo
uliofanyika Arusha Oktoba mwaka huu ambapo moja ya maazimio ni waajiri kuwapa
fursa wafanyakazi wao kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii. Katikati ni Meneja
Uwekezaji wa mfuko huo Selestine Some na Mwishoni ni Ofisa Habari wa Idara
ya Habari (MAELEZO) Bi. Fatma Salum.
Meneja Huduma kwa Wateja na Wanachama wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF Godfrey Mollel akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo
pichani) mpango wa mfuko huo kufikisha wanachama 400,000 ifikapo mwaka 2015,
kwa sasa mfuko huo una wanachama takribani 300,000, kushoto ni Meneja Uhusiano
na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria
mkutano na Mfuko wa Pensheni wa PPF katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
jana Jumatatu jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Silayo - MAELEZO
Na Hassan
Silayo - Maelezo
Waajiri nchini
wametakiwa kuwa utaratibu wa kutoa mafunzo elekezi kwa waajiriwa
kuhusu namna ya kujiandaa na maisha ya kustaafu tangu siku mfanyakazi
anapoingia katika ajira.
Wito huo umetolewa na Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) Lulu Mengele wakati wa mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika jana Jumatatu jijini Dar es Salaam.
Megele alisema
kuwa kumekuwa na tabia ya waajiriwa kusahau kujiwekea akiba na hivyo
kusababisha matatizo wakati wa kustaafu.
“Napenda kuwaasa waajiri waanzishe utaratibu wa
kutoa mafunzo elekezi kuhusu namna ya kujiandaa na maisha ya kustaafu tangu
siku mfanyakazi anapoingia katika ajira hii itamsaidia mfanyakazi kuwa na
mipango ya maandalizi kabla ya kustaafu na sio kusubiri mtu astaafu ndio aanze
kuweka mipango ya maisha yake,” Alisema Mengele.
Pia Menegele
aliongeza kuwa kuna haja ya waajiri nchini kuwapa fursa Wafanyakazi wapya
kujiunga na Mifuko mbalimbali ya Hifadhi ya Jamii.
“Napenda kuwaasa waajiri wote nchini kuwapa fursa wafanayakazi
wapya kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwani kwa kufanya hivi kutaweza
kuwasaidia wafanyakazi kuwa na uwezo wa kujikimu na kukabiliana na changamoto
za maisha katika siku za baadae,” alisema.
Akieleza mipango ya kuongeza wanachama meneja wa
huduma kwa wateja na wanachana Godfrey Mollel alisema wanamipango ya kuongeza
wanachama hadi kufikia 400,000 ifikapo mwaka 2015.
“Kwa sasa tuna wanachama 300,000 lakini kutokana na
ubora wa huduma za PPF tunategemea kuongeza idadi ya wanachama hadi kufikia 400,000
ifikapo mwaka 2015.
Mfuko wa Pensheni wa PPF unajivunia kutekeleza
majukumu yake kwa asilimia 80 kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na
Mwasiliano (TEHAMA).
No comments:
Post a Comment