Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (wapili kulia) akitoa ufafanuzi wa
masuala mbalimbali ya adhabu mbadala ya kifungo gerezani kwa waandishi wa
habari baada ya kufungua mkutano wa siku tatu wa masuala wa adhabu mbadala wa
kifungo gerezani katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Holiday Inn, jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini
Malemi, ambaye alimwakilisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel
Nchimbi katika mkutano huo. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma
kwa Jamii, Fidelis Mboya, na kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendelezaji wa
Magereza wa Jeshi la Magereza, Dk Juma Malewa. Mkutano huo umeandaliwa na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Huduma kwa Jamii, kwa
kushirikiana na Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na Maboresho ya Sheria
za Adhabu la Penal Reform International. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi, akiisoma
hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ambaye
alimuakilisha katika mkutano wa siku tatu wa masuala wa adhabu mbadala wa
kifungo gerezani unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Holiday
Inn, jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed
Chande Othman ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo
uliojumusiha nchi ya Ethiopia, Kenya, Malawi, Rwanda, Afrika Kusini, Sudani ya
Kusini, Uganda, Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania. Kulia ni Jaji wa Mahakama
Kuu nchini, Shabani Lila na Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Jamii,
Fidelis Mboya. Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
kupitia Idara ya Huduma kwa Jamii, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa
linalojishughulisha na Maboresho ya Sheria za Adhabu la Penal Reform
International. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wacheza
ngoma wa Jeshi la Magereza, Dar es Salaam, wakitoa burudani kwa washiriki wa
mkutano wa masuala wa adhabu mbadala wa kifungo gerezani unaofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Holiday Inn, jijini Dar es Salaam. Jaji Mkuu wa
Tanzania, Mohamed Chande Othman aliufungua mkutano huo unaojumusha nchi ya
Ethiopia, Kenya, Malawi, Rwanda, Afrika Kusini, Sudani ya Kusini, Uganda,
Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania. Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Huduma kwa Jamii, kwa kushirikiana na
Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na Maboresho ya Sheria za Adhabu la
Penal Reform International. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Baadhi
ya washiriki kutoka nchi ya Ethiopia, Kenya, Malawi, Rwanda, Afrika Kusini, Sudani
ya Kusini, Uganda, Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania wakiwaangalia wacheza
ngoma waliokuwa wanatumbuzia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu unaojadili
masuala ya adhabu mbadala ya kifungo gerezani unaofanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Hoteli ya Holiday Inn, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo
umeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Huduma kwa
Jamii, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na
Maboresho ya Sheria za Adhabu la Penal Reform International. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (watatu kushoto-waliokaa), Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (katikati-waliokaa)
wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa kutoka nchi
ya Ethiopia, Kenya, Malawi, Rwanda, Afrika Kusini, Sudani ya Kusini, Uganda,
Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania. Mkutano huo ambao umeandaliwa na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Huduma kwa Jamii, kwa kushirikiana
na Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na Maboresho ya Sheria za Adhabu la
Penal Reform International umefunguliwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya
Holiday Inn, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
No comments:
Post a Comment