Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 29 November 2013

PIMAJOTO KUELEKEA 2015: PROFESA JUMA ATHUMANI KAPUYA WA URAMBO MAGHARIBI

 Profesa Juma Kapuya. Picha kwa hisani ya Global Publishers Limited.

Na Daniel Mbega

HUU ni mfululizo wa makala zitakazokuwa zikichambua wabunge na majimbo mbalimbali kuona kama bado wapigakura wanawahitaji wawakilishi wao hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko. Wapo wabunge waliokaa Bungeni zaidi ya miaka 10, hivyo uga huu unatoa fursa kwenu wasomaji kutoa maoni kama bado wanastahili kuendelea au wanapaswa kuwapisha wengine.
Kwa bahati njema, pimajoto yetu inaanza na Profesa Juma Athumani Kapuya, Mbunge wa Jimbo la Urambo Magharibi mkoani Tabora.
Profesa Kapuya (68) ni miongoni wanasiasa wakongwe nchini ambaye alianza kujihusisha na siasa tangu akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1971.
Anamalizia kipindi cha nne cha ubunge tangu alipoingia Bungeni mwaka 1995 alipoachana na uprofesa wa mimea pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ni miongoni mwa wabunge waliopata bahati ya kuingia kwenye Baraza la Mawaziri katika kipindi cha kwanza tu wakati alipoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni.
Hapa anakumbukwa vyema kutokana na wapenzi wa soka kutokana na ‘kuivuruga’ Ligi Kuu mwaka 1999 baada ya kuagiza timu za Milambo ya kwao Tabora na CDA zilizokuwa zimeshuka daraja, zisishuke. Badala yake akaagiza mfumo mpya wa ligi utumike. Hii iliuwa ni baada ya kubariki rufaa za timu hizo zilizopinga kushushwa daraja msimu wa 1998.
Milambo ikaokolewa pia mwaka 1999 isishuke daraja pamoja na kushika mkia nyuma ya Toto African, hivyo kuifanya ligi ya mwaka 2000 kuwa na timu 20 baada ya nne kupanda msimu huo.
Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, Profesa Kapuya aliyezaliwa Juni 22, 1945, akabahatika tena kuwa bosi wa michezo wakati alipoteuliwa kuwa Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo, ambayo ilitolewa kwenye Wizara ya Elimu na Utamaduni. Aliiongoza wizara hiyo hadi mwaka 2005.
Januari Mosi, 2006 aliteuliwa katika serikali ya awamu ya nne kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa aliyodumu nayo hadi Februari 8, 2008 wakati Rais Jakaya Kikwete alipolivunja Baraza la Mawaziri kufuatia kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Edward Lowassa. Siku tano baadaye akarudishwa kwenye Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana alikodumu hadi mwaka 2010.
Wakati akiwa Waziri wa Ulinzi iliwahi kudaiwa kwamba alitumia vibaya madaraka yake kwa kutumia ndege ya jeshi kwenda jimboni kwake.
Mwanasiasa huyo mkongwe yuko kwenye wakati mgumu kurejea Bungeni 2015 kufuatia kashfa ya ubakaji anayodaiwa kuifanya kwa binti wa miaka 16 na yaliyoendelea kila mmoja anajua. Kwa vile mheshimiwa mwenyewe amevishtaki baadhi ya vyombo vya habari kuhusu suala hilo, sitapenda kuingia kwa undani kwa vile itakuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama.
Elimu ya msingi aliipata katika shule za Kaliua N.A (1954 hadi 1957) na Sikonge Middle School (1958 hadi 1961). Akajiunga na shule ya sekondari Tabora Boys (1962 hadi 1965) kabla ya kuendelea na kidato cha tano na sita katika shule hiyo hiyo (1966 hadi 1967).
Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuchukua Shahada ya Elimu (1968 hadi 1971) akachukua shahada ya uzamili katika Mimea kwenye chuo hicho (1971 hadi 1972), kabla ya kuchukua shahada ya uzamivu (PhD) katika Mimea kutoka Chuo Kikuu cha Wales Aberystwyth (1972 hadi 1975).
Aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Sukari, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Tumbaku, Mshauri wa TYL na UVCCM wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwaka 1971 hadi 1974 alikuwa Mkufunzi Msaidizi wa Mimea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akawa Mhadhiri Msaidizi (1974 hadi 1976), Mhadhiri kamili (1976 hadi 1978), Mhadhiri Mwandamizi (1978 hadi 1983), Profesa wa Mimea (1983 hadi 1995).
Wajumbe mnao uhuru wa kuchangia maoni yenu, ikiwezekana kupitia barua-pepe brotherdanny5@gmail.com au ujumbe (meseji) kupitia 0655-220404.

Wasifu wake kamili ni huu:
Member of Parliament CV
GENERAL
Salutation
Honourable

First Name:
Prof. Juma
Middle Name:
Athumani
Last Name:
Kapuya
Member Type:
Constituency Member
Constituent:
Urambo Magharibi
Political Party:
CCM
Office Location:
P.O. Box 11365, Dar es Salaam
Office Phone:
+255 784 993930/+255 776 784185
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail:
Member Status:
Current Member
Date of Birth
22 June 1945

EDUCATION
School Name/Location
Course/Degree/Award
Start Date
End Date
Level
University College of Wales Aberystwyth
PhD (Botany)
1972
1975
PHD
University of Dar es Salaam
MSc. (Botany)
1971
1972
MASTERS DEGREE
University of Dar es Salaam
BSc. (Education) Hons
1968
1971
GRADUATE
Katholicke University, Nijmegen
Certificate
1982
1983
CERTIFICATE
International Atomic Energy Agency
Certificate
1986
1986
CERTIFICATE
Tabora Boys Secondary School
A-Level Education
1966
1967
HIGH SCHOOL
Tabora Boys Secondary School
O-Level Education
1962
1965
SECONDARY
Kaliua Primary School
Primary Education
1954
1957
PRIMARY
Sikonge Middle School
Primary Education
1958
1961
PRIMARY
Ads not by this site
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name
Position
From
To
Ministry of Defence & National Serv.
Minister
2006
2/8/2008
Ministry of Labour, Employment and Youth Development
Minister
2/13/2008
2010
The Parliament of Tanzania
Member - Urambo West Constituency
1995
2015
University of Dar es Salaam
Professor of Botany
1987
1995
University of Dar es Salaam
Associate Professor(Botany)
1983
1987
University of Dar es Salaam
Senior Lecturer(Botany)
1978
1983
University of Dar es Salaam
Lecturer(Botany)
1976
1978
University of Dar es Salaam
Assistant Lecturer(Botany)
1974
1976
University of Dar es Salaam
Tutorial Assistant(Botany)
1971
1974

POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location
Position
From
To
Chama Cha Mapinduzi - CCM
Member of National Executive Council (NEC)
1997
Todate
Chama Cha Mapinduzi - CCM
Ten Cells Leader(Darajani) - UDSM
1983
1995
Chama Cha Mapinduzi - CCM
Ambassodor
1977
1997
TANU-Tanganyika Youth League(University of DSM)
Advisor/Member
1972
1977

No comments:

Post a Comment