Karibu maiti 400 zilizoanza kuharibika nchini Ufilipino zimezikwa kwenye mtaro huku maiti 393 zikiwa hazijatambuliwa.
Hali hiyo imetokana na maafa makubwa ya kimbunga cha Haiyan kilichotokea huko Ufilipino wiki iliyopita ambapo maiti hizo zilikuwa zimewekwa kwenye mifuko ya plastiki.
Hali hiyo imetokana na maafa makubwa ya kimbunga cha Haiyan kilichotokea huko Ufilipino wiki iliyopita ambapo maiti hizo zilikuwa zimewekwa kwenye mifuko ya plastiki.
Maiti zilizotambuliwa hazifiki hata 60, kwa mujibu wa taarifa kutoka huko, ambapo zaidi ya watu 4,000 wamefariki dunia mpaka sasa katika kisiwa cha Tacloban kilikotokea kimbunga Haiyan.
Meya wa Tacloban, Alfred Romualdez alisema maiti nyingi zitakuwa zimesombwa na maji kupelekwa baharini na haziwezi kupatikana.
Eneo moja lililokuwa na wakazi kati ya 10,000 na 12,000 halikuwa na watu kabisa, alisema.
Kila mahari kwenye mji huo kulikuwa na maiti zilizoanza kuoza, hivyo kutolewa uamuzi wa kuzika haraka ili kuepusha kuenea kwa magonjwa hasa baada ya vyumba vya kuhifadhia maiti kubomolewa na dhoruba hiyo.
No comments:
Post a Comment