Ndugu zangu,
Kimsingi napenda sana historia, niliipenda tangu nikiwa mtoto, tangu wakati nilipokuwa nasimuliwa hadithi. Tabia ya kupenda kujikumbusha mambo ya zamani ninayo na nitaendelea nayo, ndiyo maana nafanya utafiti wa historia, japokuwa sijasomea historia.
Naam, enzi zile nilipenda kusoma kuhusu mashujaa mbalimbali wa Afrika. Eduardo Chivambo Mondlane rais wa kwanza wa Chama cha Ukombozi cha Msumbiji (Frente de Libertação de Moçambique au FRELIMO) ambaye aliuawa Februari 3, 1969 na Samora Moises Machel mkuu wa majeshi ya FRELIMO aliyerithi mikoba ya Mondlane, ni miongoni mwa mashujaa ninaowaheshimu sana.

Nilipokuwa Msumbiji nilipata bahati ya kutembelea makumbusho ya FRELIMO katika Kijiji cha Congresso, wilaya ya Matcheje mkoani Lichinga.
Hakika nilifurahi sana, kwa sababu hapo ndipo mahali FRELIMO walipofanyia mkutano wao wa pili Julai 1968 baada ya ule wa Dar es Salaam kabla ya kuanzisha harakati za kumng'oa Mreno.
Nilibahatika pia kukalia gogo ambalo Mondlane alikuwa akikaa na Machel kupanga mikakati ya vita, walikuwa wakikaa wawili tu, peke yao. Na gogo lenyewe lingali mpaka sasa kama linavyoonekana.
Historia ina manufaa makubwa sana kwa vizazi vyetu.
Ndugu yenu,
Daniel Mbega
No comments:
Post a Comment