Wayne Rooney (26)
MHUDUMU wa mapokezi katika jumba la
upunaji (massage
parlour) anayedaiwa kufanya mapenzi na Wayne Rooney alimwambia mwanandinga huyo aondoke mara moja 'kabla hajachafuliwa na soka yake
kwisha', mahakama ya Old Bailey ilielezwa Jumatatu.
Patricia Tierney, 58, alikanusha
kulipwa fedha ili afanye mapenzi na mwanandinga huyo katika danguro la mjini Liverpool mwaka 2004, kufuatia msururu wa taarifa kuhusu Rooney
‘kufanya mapenzi na makahaba', mahakama iliambiwa.
Mama huyo mwenye watoto saba alisema
katika hati yake ya maelezo kwamba alihofia hatma ya mshambuliaji huyo wa
Manchester United wakati alipomwendea kwa mara ya pili akitaka kufanya naye
mapenzi baada ya kunogewa, na akamtaka aondoke haraka.
“Tukio hilo, ambalo ni la uongo,
inadaiwa kwamba nilifanya mapenzi na Wayne Rooney na kwamba alinilipa katika
siku isiyofahamika wakati nikifanya kazi kwenye jumba la upunaji,” alisema.
“Nakumbuka Wayne Rooney alikuja
pamoja na wanaume wengine. Siku kadhaa baadaye alikuja peke yake. Safari hii
nilimsukumia kwenye chumba na kumwambia avute kofia yake kuficha uso na aondoke
haraka kabla hajachafuliwa na kumaliza soka yake.”
Glenn Mulcaire wa gazeti
lililofungiwa la News of the World ambaye alikuwa anamchunguza Wayne Rooney wakati
huo, alikutwa na jina na tarehe ya kuzaliwa ya Tierney kwenye nyaraka zake,
mahakama iliambiwa.
Karatasi nyingine zilizokutwa
nyumbani kwake zilionyesha kwamba jina la siri la simu ya Wayne Rooney lilikuwa
Stella Artois.
Habari nyingine kwenye kompyuta
iliyoandikwa 'Project Patricia Tierney' ilikutwa kwa mwandishi huyo.
“Ninaamini hii inahusiana na tukio
la kwenye danguro,” alisema Tierney, akaongeza: “Nilipewa Pauni 30,000 (na News
of the World) kwa ajili ya habari hiyo lakini nikakataa.”
Notebook za Mulcaire, ambaye alikuwa
anaingilia mawasiliano ya siri ya Rooney, zilikubwa na taarifa zinazomhusu mama
wa Rooney, mahakama iliambiwa.
Siku nyingine aliandika dokezo la
taarifa za simu kuhusu mwanamitindo aitwaye Laura Rooney. Wiki iliyopita
ilibainika kwamba alikuwa anamfuatilia mwanadada huyo kwa makosa akidhani
kwamba ana udugu na mshambuliaji huyo wa Manchester United na England.
Mwendesha mashtaka Andrew Edis QC aliiambia
mahakama: “Simu ya Laura Rooney ilitegwa na mawasiliano yake kunaswa kwa sababu
walidhani ana udugu na Wayne Rooney, ambaye simu yake pia ilikuwa imetegwa ili
kunasa mawasiliano yake. Hakuwa na udugu wowote na Wayne Rooney na hahusiani
naye kwa lolote. Ni mtengeneza nywele ambaye hamfahamu Wayne Rooney lakini
akajikuta akichunguzwa kama tu alikuwa na uhusiano naye.”
Mtendaji mkuu wa zamani wa News
International Rebekah Brooks, 45, kutoka Churchill, Oxfordshire; daktari wa
zamani Andy Coulson, pia mwenye miaka 45, kutoka Charing huko Kent; mkuu wa
habari wa News of the World Ian Edmondson, 44, kutoka Raynes Park, kusini
magharibi mwa London; na mhariri mtendaji wa zamani wa gazeti hilo Stuart
Kuttner, 73, kutoka Woodford Green, Essex, wote wanashtakiwa kwa kushirikiana
na wengine kuingilia mawasiliano ya simu za watu kati ya Oktoba 3, 2000 na
Agosti 9, 2006.
Kesi hiyo bado inaendelea.
Chanzo: dailymail.co.uk
No comments:
Post a Comment