Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi
JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Simu: +255-22-2112035/40
|
S.L.P. 9223
|
|
Nukushi: +255-2122617/2120486
Barua Pepe: ps@moha.go.tz
|
Dar es Salaam
|
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kutokana
na Maboresho yanayoendelea ndani ya Jeshi la Polisi kumekuwepo na mikakati
mbalimbali inayolenga uboreshaji wa
miundombinu yake, ikiwa ni pamoja na kupata ofisi, vituo vya polisi, makazi ya
kuishi askari makambini, vifaa na vitendea kazi ili kuimarisha ulinzi na
usalama nchini.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi iliona kuna umuhimu wa kuanzisha Shirika la uzalishaji mali la Polisi (Tanzania Police Corporation Sole) ili kuendelea kufanikisha malengo ya maboresho yanayoendelea.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi iliona kuna umuhimu wa kuanzisha Shirika la uzalishaji mali la Polisi (Tanzania Police Corporation Sole) ili kuendelea kufanikisha malengo ya maboresho yanayoendelea.
Kufuatia
hatua hiyo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliridhia
kuanzishwa kwa Shirika la Uzalishaji
ndani ya Jeshi la Polisi baada ya kusaini Amri ya uanzishwaji Shirika
hilo tarehe 27/9/2012 kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1974 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2000.
Mara baada ya kusainiwa na Mheshimiwa Rais,
Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kwa mujibu wa sheria ameteua Bodi
ya Shirika hili na kumteua Ndugu EMMANUEL
HUMBA kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa miaka mitatu kuanzia tarehe 19/9/2013, aidha
amewateua wajumbe wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi hiyo:-
(1)Mwakibinga E.P.M Mihalale-
Msajili wa Hazina Msaidizi
(2)Jehad Abdallah Jehad –Msajili
Bodi ya Wakadiriaji na Wasanifu
Majengo
(3) Melkior Temu- Mipango, Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi
(4) T.M.E Andengenye –DCP Mkuu wa
Utawala Jeshini
(5) A. Nyamhanga –ACP-Mkuu wa
Kitengo cha Mipango na Bajeti Jeshi la
Polisi
(6)Samwel Marco-Meneja Hazina –(Tressure)-TIB
(7) John Mathew- Kaimu
Mkurugenzi Mhamasishaji- TIC
Katika
uteuzi huo amemteua pia DCP- SOSPETER M. KONDELA kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Kwanza wa Shirika hilo .uteuzi huo unaanza mara moja.
Imetolewa na Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
18 NOVEMBA, 2013.
No comments:
Post a Comment