Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika akiwa katika Jengo la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete lililopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako amewatembelea wagonjwa wa moyo jana. Kanu atakuwepo nchini kwa muda wa siku tano kushiriki shughuli mbalimbali za kampuni na kijamii.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo katika Taasisi hiyo, Dk Peter Kisenge (kushoto) akimkaribisha Nwankwo Kanu Ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika. Kanu atakuwepo nchini kwa muda wa siku tano kushiriki shughuli mbalimbali za kampuni na kijamii.
Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika akizungumza baada ya kufika Muhimbili.
Kanu (kulia), akizungumza na madaktari wa Taasisi hiyo.
Fatuma Shaban ambaye mtoto wake anatibiwa katika taasisi hiyo akipokea zawadi kutoka kwa mchezaji huyo.
Mgonjwa katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, Mariam Omary akifurahi baada ya kupata fursa ya kutembelewa na kujuliwa hali na aliyekuwa mchezaji nyota wa nigeria, Nwanko Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika.
Mmoja wa madaktari wa taasisi hiyo (kulia), akitoa maelezo mbele ya mchezaji huyo.
Na Dotto Mwaibale
Na Dotto Mwaibale
Aliyekuwa mchezaji nguli wa timu ya taifa ya Nigeria au Super Eagles, Nwankwo
Kanu ambaye pia kwa sasa ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika jana jioni alitembelea
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa lengo la kujua ni jinsi
gani taasisi hiyo inafanya kazi pamoja na kuwajulia hali wagonjwa wa moyo
waliolazwa katika Taasisi hiyo. pia
Akizungumza baada ya kuwasili katika Taasisi hiyo Kanu ameelezea kuguswa na tatizo
la ugonjwa wa moyo hasa kwa watoto wadogo ambao amewatembelea na kuahidi
kubadilishana uzoefu kuhusu huduma za matibabu zinazotolewa na wataalamu wa
tasisi hiyo.
“Tatizo la moyo ni kubwa sana kwa sasa na limekuwa likiongezeka kwa kasi
lakini cha kusikitisha ni kuwa sio kila mtu anaweza kumudu gharama za matibabu
yake. Hivyo basi kuna umuhimu mkubwa sana kwa serikali na wadau wengine
kuanzisha vituo maalumu kama hivi ili kuwasaidia wasiojiweza.” Alisema Kanu
Katika mazungumzo yake mchezaji huyo wa nyota wa zamani ambaye aliwahi
kuwika na vilabu kama vile vya Arsenal, Ajax na Inter Milan, amesema kuwa
pamoja na kuja kwa shughuli mbalimbali kama balozi wa kampuni ya StarTimes
lakini pia ana nia ya kushirikiana na watalaamu wa Taasisi hiyo ya Moyo.
Alielezea kuwa lengo ni kuwasaidia matibabu watoto wenye matatizo ya Moyo ambao
wazazi wao hawana uwezo na kwamba watazungumzia suala hilo.
“Nimefarijika sana kuona serikali ya watu wa Tanzania inachukua hatua
stahiki katika kuwasaidia wananchi wake. Pia ningependa kuchukua fursa hii
kuwataka watanzania hasa wanamichezo kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara
kwa mara kwani ukijua tatizo mapema ni rahisi kupata matibabu na kupona.
Tumeona mifano michache ya wachezaji maarufu mbalimbali barani Afrika na
kwingineko duniani wakifariki au kunusurika kufa wakiwa katika ya mchezo
kutokana na kutoweka wazi mustakabali wa afya zao.” Alihitimisha balozi huyo wa StarTimes barani Afrika
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji kwa watoto kutoka Taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete, Dk. Godwin Godfrey amelezea kuwa tangu Julai mwaka
jana mpaka sasa tasisi hiyo kwa kushirikiana na wataalam kutoka nje ya nchi
wamewafanyia upasuaji watoto zaidi ya 200.
Nwankwo Kanu mbali na kujizolea umaarufu na heshima kubwa katika medani
za soka barani Afrika na Ulaya yeye pia alifanyiwa upasuaji wa moyo mwaka 1996 na ndipo alipoamua kufungua taasisi yake ya moyo inayoitwa “The Kanu Heart Foundation.”
Taasisi yake hiyo iliyoko nchini Nigeria ambako ndiko alipozaliwa
aliianzisha kwa madhumuni makubwa ya kusaidia wenye matatizo kama yake na
ameahidi taasisi hiyo kushirikiana na taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika
masuala mbalimbali.
No comments:
Post a Comment