Mwesigwa ametoa msimamo huo leo baada ya gazeti hilo kuchapisha habari inayodai alikuwa miongoni mwa waliohudhuria kikao cha upangaji matokeo ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
"Nimeshtushwa na kusikitishwa sana na habari hiyo juu yangu ambayo ni ya kutunga, yenye nia mbaya isiyokuwa ukweli wowote, kwani sijawahi kukaa na watu wowote kupanga njama yoyote iliyo kinyume na maadili ya mchezo wa mpira wa miguu " alisema Mwesigwa.
Gazeti la Tanzania Daima toleo nambari 4143 la leo tarehe 7 Aprili 2016 lilichapisha habari katika ukurasa wake wa 24 chini ya kichwa cha habari " Vigogo TFF wajikaanga" likisema katika ibara ya 7 kuwa kwenye mazungumzo yaliyochukua zaidi ya dakika 10 yalihusisha pia Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa.
No comments:
Post a Comment