Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG), Profesa Juma Assad akionesha ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa
fedha unaoishia Juni 30, 2015 kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo
mjini Dodoma ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka
2016/2017.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG), Profesa Juma Assad akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani) leo mjini Dodoma juu ya ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia
Juni 30, 2015 ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka
2016/2017.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad
akiongea na waandishi wa habari leo mjini Dodoma juu ya ripoti ya ukaguzi ya
mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 ili iweze kujadiliwa na wabunge katika
Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.
Waandishi wa habari wakipokea ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia
Juni 30, 2015 ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka
2016/2017.
Picha
na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Na
Eleuteri Mangi-MAELEZO
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad amekabidhi
ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 bungeni leo ili
iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.
Katika
ripoti yake, CAG ametoa mapendekezo kadhaa ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili
kuboresha matumizi ya fedha za Serikali kwa malengo yanayokusudiwa.
Miongoni
mwa maeneo ambayo CAG ametoa mapendeklezo ni Ofisi ya Masjili wa Vyama vya
Siasa nchini ifuatilie suala la uwasilishaji wa taarifa za fedha kwa wakati
kulingana na matakwa ya sheria.
Hatua
hiyo ya CAG inafuatia ukaguzi uliofanywa kwenye vyama vya siasa nchini vyenye
usajili wa kudumu ambavyo jumla yao ni vyama 22.
Prof.
Assad alisema kuwa kati ya vyama hivyo vyenye usajili wa kudumu, ni chama
kimoja ndicho kilichowasilisha hesabu zake kwa kipindi cha miezi sita kuanzia
Januari hadi Juni 2015 ambacho ni Chama cha Wananchi (CUF).
Vyama
vingine 21 havikuwasilisha vitabu vya hesabu kwa ajili ya ukaguzi kinyume cha
kifungu Na. 14 cha Sheria ya vyama vya siasa Na. 5 ya mwaka 1992.
No comments:
Post a Comment