Mratibu wa Heart Marathon Dkt. Omary Chillo (katikati)
akiongea na waandishi wa habari kuhusu
mashindano ya mbio maalum za kupambana na ongezeko la magonjwa
yasiyoambukiza zijulikanazo kama Heart Marathoni zinazotarajiwa kufanyika
Aprili 26 mwaka huu jijini Dar es salaam, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart Marathon
Dkt. Chaka Halfani na kulia kwake ni Kaimu Katibu Chama cha Riadha
Tanzania Bi. Ombeni Zavala.
Mratibu wa Heart Marathon Dkt. Omary Chillo (wa kwanza kulia) akiongea na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya mbio maalum za kupambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza zijulikanazo kama Heart Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu jijini Dar es salaam, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart Marathon Dkt. Chaka Halfani na Mratibu Msaidizi Heart Marathon Bi.Catherine ikangaa.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart Marathon
Dkt. Chaka Halfani akionyesha kwa waandishi wa habari namba watakazopewa washiriki wa mbio maalum
za kupambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza zijulikanazo kama Heart
Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu jijini Dar es salaam,kulia
kwake ni.Mratibu wa Heart Marathon Dkt.
Omary Chillo na Kaimu Katibu Chama cha Riadha Tanzania Bi.Ombeni Zavala .
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart Marathon
Dkt. Chaka Halfani akionyesha kwa waandishi wa habari fulana watakazovaa washiriki wa mbio maalum
za kupambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza zijulikanazo kama Heart
Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu jijini Dar es salaam,kulia
kwake ni.Mratibu wa Heart Marathon Dkt.
Omary Chillo.(Picha na Lorietha Laurence-Maelezo).
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Taasisi ya Tanzania Health Summit imeandaa mbio maalumu za kupambana na ongezeko la magonjwa yasioambukiza yajulikanayo kama Heart Marathon zitakazofanyika Aprili 26, 2016 katika viwanjwa vya michezo vya Chuo Kikuu jijini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa na Mratibu Kamati ya Maandalizi ya Mbio hizo Dkt. Omary Chillo ambapo amesema kuwa lengo lake ni kusaidia juhudi za Serikali na wadau wa Sekta ya Afya kupunguza tatizo linalokuwa kwa kasi la magonjwa yasioambukizwa hapa nchini.
“Watanzania wote kwa ujumla tunawaalika kushiriki katika mbio za Heart Marathon zitakazoambatana na upimaji wa magonjwa yasiyoambukizwa na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa ugonjwa wa Kisukari, Shinikizo la Damu, Uwiano wa urefu na uzito, wingi wa mafuta mwilini pamoja na Saratani ya matiti” alisema Dkt. Chillo.
Amesema mbio hizo zinatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 2,000 kutoka taasisi, makampuni, mashirika, familia na jamii kwa ujumla, rika tofauti ikiwemo watoto, vijana na wazee, makundi ya walemavu na watu wenye magonjwa yasioambukiza watashiriki.
Aidha, Dkt. Chillo ameongeza kuwa mbio hizo zimegawanywa kwa umbali tofauti ambazo ni mbio ndefu za Kilometa 21.1 kwa ajili ya wakimbiaji wazoefu, kilometa 10 kwa wakimbiaji wa kati, Kilometa 5 wakimbiaji wa kawaida, kifamilia na kampuni pamoja na mbio za watoto chini ya miaka 12 watakimbia umbali wa mita 700.
Kauli mbiu kwa mwaka huu katika mbio maalumu za kupambana na ongezeko la magonjwa hayo ni “Epuka magonjwa yasioambukiza”
Viingilio katika mbio hizo maalumu zitakuwa kuanzia elfu tano kwa watoto wa chini ya umri wa mika 13 hadi Shilingi 10,000 kwa mtu mmoja ambapo watu wenye ulemavu hawatalipia kiingilio.
No comments:
Post a Comment