Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine (katikati) akimkabidhi jezi
ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Balozi wa StarTimes barani Afrika Nwankwo
Kanu kutoka nchini Nigeria, lengo ni kuthamini mchango wake.Kulia ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania,
Lanfang Liao.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine, akizungumza na wadau wa
mpira nchini kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kampuni ya
StarTimes kwa lengo la kumkaribisha Balozi wa StarTimes barani Afrika Nwankwo
Kanu kutoka nchini Nigeria.
Balozi wa StarTimes barani
Afrika Nwankwo Kanu akizungumza na wadau wa mpira nchini kwenye hafla ya
chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kampuni ya StarTimes kwa lengo la
kumkaribisha nchini mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Na
Eleuteri Mangi-MAELEZO
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine ameishukuru Kampuni ya StarTimes
Tanzania kwa kuthamini soka kwa kumleta nchini mchezaji nguli wa kimataifa wa
Nigeria, Nwanko Kanu.
Mwesiga aliyasema hayo mwishoni mwa
wiki jijini Dar es salaam kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na
Kampuni ya StarTimes kwa lengo la kumkaribisha Balozi wa StarTimes barani
Afrika Nwankwo Kanu kutoka nchini Nigeria.
“Kupitia
StarTimes tutaboresha mpira wetu kwa kuangalia ligi mbalimbali za mataifa ya
Ujerumani, Italia na Ufaransa” alisema Mwesigwa.
Ujio wa Kanu nchini ni fursa na
unamanufaa makubwa kwa mustakabali wa ukuaji wa soka hasa kwa kuzingatia afya
ya vijana katika michezo.
Kwa upande wake Balozi wa StarTimes
barani Afrika Nwankwo Kanu ambaye alikuwa mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Nigeria
(Super Eagles) amesema kuwa amekuja Tanzania kwa mwaliko wa StarTimes na kuahidi
kurudi kwa shughuli zake za kimichezo maana amefurahishwa na mapokezi na
anaamini mchango wake katika soka la Tanzania unahitajika.
“Mustakabali wa mpira wa miguu wa
Tanzania utakuwa mkubwa kama Watanzania watapenda kufuatilia masuala ya mpira
wa miguu kupitia ligi tofauti tofauti, kadiri unavyoangalia michezo mbalimbali
ya kimataifa, ndivyo unavyozidi kujifunza” alisema Kanu.
Kanu alifanyiwa upasuaji wa moyo mwaka
1996 na ndipo alipoamua kufungua taasisi yake ya moyo inayoitwa “The Kanu Heart
Foundation.”
Taasisi hiyo iliyoko nchini Nigeria
ambako ndiko alipozaliwa aliianzisha kwa madhumuni makubwa ya kusaidia wagonjwa
wenye matatizo ya moyo na ameahidi taasisi hiyo kushirikiana na taasisi ya Moyo
ya Jakaya Kikwete katika masuala mbalimbali ya kitabibu.
Kanu mbali na kuchezea timu yake ya
Taifa, pia aliwahi kuchezea vilabu vya Iwuanyanwu Nationale kati ya mwaka 1992
hadi 1993, mwaka 1993 hadi 1996 alichezea
AFC Ajax, mwaka 1996 hadi 1999 alichezea Inter Milan, mwaka 1999 hadi 2004
aliichezea Arsenal, mwaka 2004 hadi 2006 alichezea West Bromwich Albion na mwkaa 2006 hadi 2012 alichezea
Portsmouth.
No comments:
Post a Comment