Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi Angelina Kairuki akisisitiza jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mchakato unaoendelea wa kubaini
watumishi hewa Serikalini, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Utumishi Angelina Kairuki alipokutana na waandishi wa habari kuelezea mchakato
unaoendelea wa kubaini watumishi hewa Serikalini, mapema hii leo jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimali Watu toka Ofisi ya Rais
Utumishi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi Angelina Kairuki alipokutana na waandishi
wa habari kuelezea mchakato unaoendelea wa kubaini watumishi hewa Serikalini,
mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Utumishi Angelina Kairuki wakati akielezea
mchakato unaoendelea wa kubaini watumishi hewa Serikalini, mapema hii
leo jijini Dar es Salaam.
Picha
zote na Eliphace Marwa - Maelezo
Na Jacquiline
Mrisho-MAELEZO
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bibi
Angela Kairuki amewapa wiki moja waajiri wa sekta za umma nchini kukamilisha na
kuwasilisha taarifa kuhusu watumishi hewa.
Bibi
Kairuki ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokua akiongea na waandishi
wa habari kuhusu taarifa za awali juu ya watumishi hewa zilizowasilishwa na
Wakuu wa Mikoa nchini.
Hadi
sasa taarifa hizo za Mikoa zimebaini jumla ya watumishi hewa 1830 ambapo idadi
hiyo inazidi kuongezeka kadri utafiti unavyondelea kufanyika.
“Tunatumia
zaidi ya asilimia 51 ya pato la ndani kwa ajili ya mishahara na stahiki za
wafanyakazi wa Serikalini, sasa kama waajiri hawatowataja na kuwasilisha
watumishi hewa tutazidi kupoteza pato la Taifa, Ofisi imewaagiza waajiri wote
kuwasilisha taarifa zao wiki hii ili kuiwezesha ofisi hii na Serikali kiujumla
ili kujua kwa usahihi watumishi hewa ni wangapi na hatua zinazoendelea kuchukuliwa
na mamlaka hizo za ajira” alisema Bibi Kairuki.
Waziri
Kairuki ameongeza kuwabaada ya ukusanyaji wa watumishi hewa kuisha, ofisi yake
itafanya ukaguzi kwenye sekta zote za umma nchini ili kuhakikisha watumishi
hewa wote wanaondolewa pia waajiri watakaokua
hawajawawasilisha watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha,Bibi
Kairuki amesisitiza kuwa jukumu la kuwaondoa watumishi sio la ofisi ya Utumishi
bali ni dhamana aliyopewa mwajiri wa
sehemu husika. Hivyo amewataka waajiri kutimiza wajibu wao.
Amewataka
waajiri waambatanishe vielelezo vilivyokosekana katika taarifa za awali za
watumishi hewa vikiwemo; majina, vyeo vyao, vituo vya kazi, namba zao za
utambulisho (Check No) pamoja na sababu za kuwaondoa katika orodha ya malipo.
Hatua
hii imefanyika baada ya agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli alilolitoa Machi 15 mwaka huu alipokua akiwaapisha Wakuu wa
Mikoa.
No comments:
Post a Comment