Miss Tanzania 1998, Basila Mwanukuzi akiwa na Hashim Lundenga katika mkutano na wanahabari mwaka 1998.
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
MH.UMMY
MWALIMU AZINDUA RASMI TAASISI YA BASILLA
MWANUKUZI
- Yaanza na mradi wa
‘Wezesha Mama Lishe Tanzania’
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Tanzania, Ummy
Mwalimu, kesho (11.4.2016) leo amezindua rasmi
taasisi ya Basilla Mwanukuzi yenye lengo la kushirikiana na wadau ili
kuwawezesha wanawake na kuinua uwezo wao wa kibunifu na kiuchumi.
Taasisi ya BMF itajikita
katika kuwasaidia wanawake wa makundi tofauti kujitoa kutoka kwenye hali ya
kusaidiwa hadi kuweza kusimamia miradi yao wenyewe na hivyo kubadili hali zao
za maisha na kiuchumi.
Kama sehemu ya uzinduzi
wa taasisi, BMF pia imezindua mradi wa ‘Wezesha Mama Lishe Tanzania’ ukiwa na
lengo la kuwawezesha mama lishe kwa kuwawezesha kupata elimu ya ujasiriamali,
afya pamoja na kupika chakula bora chenye kuzingatia virutubisho na uwezeshaji
wa kupata mikopo na kuongeza mitaji yao.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi
huo, Mwanzilishi wa taasisi ya BMF, Basilla Mwanukuzi alisema taasisi yake
iliguswa na changamoto nyingi zinazolikabili kundi hili la mama lishe kwa
kipindi kirefu bila msaada wowote.
‘Baada ya kufanya utafiti
kwa muda mrefu na kuzungumza na Mama lishe tumegundua kina mama hawa katika
mazingira yao tofauti ya kazi wana changamoto zinazofanana kama mazingira
mabovu ya kazi na ukosefu wa mitaji, kwa hiyo mradi huu utajikita kuwasaidia
kina mama lishe watambulike, waweze kujiamini na kupewa thamani katika jamii’
alisema Basilla.
Akielezea zaidi kuhusu
mradi wa ‘Wezesha Mama Lishe’, Basilla alisema anaamini mama Lishe wakipata
mikopo wataweza kuboresha biashara zao kwa kuandaa mazingira yao ikiwa ni
pamoja na kununua viti, meza na vyombo vya kisasa vitavyowafanya wateja
wawaamini zaidi na kuwapa thamani zaidi, hivyo kubadilisha mawazo hasi katika
jamii kuwa mama lishe hawapiki chakula bora.
‘Nusu ya nguvu kazi ya
taifa inalishwa na kina mama hawa, hivyo kuna haja kubwa kuwasaidia
kurasimimisha shughuli hii, kwanza kuwasaidia kujiinua kiuchumi na pia
kuchangia pato la taifa kwa kulipa kodi na kadhalika, lakini pia vyakula vya
mama lishe ni tegemeo la watanzania wengi kwani bei yake huwa ni nafuu’ alisema
Basilla.
Utekelezaji wa Mradi wa
Wezesha Mama Lishe pia utajumuisha uundaji wa vikundi vya ushirikiano wa mama
lishe ili kubadilishana uzoefu na pia uanzishaji wa shughuli za kujiingizia
kipato kwa Mama Lishe kama utafutaji wa tenda za kuandaa vyakula vya harusi na
kadhalika.
Mpaka sasa mradi wa
Wezesha Mama Lishe umefanikiwa kuanza kuwaandikisha Mama lishe waliopo jijini
Dar es Salaam, na baadhi wameanza kupata mikopo ya riba ndogo, huku ukitarajia
kupanuka nchi nzima ili kuwafikia mama lishe wengi zaidi.
‘Hatua ya kwanza ni
kuwatambua mama lishe, ambapo mpaka sasa tuko kwenye hatua ya kuwasajili,
halafu baada ya hapo ni kutoa elimu ya afya na ujasiriamali sambamba na utoaji
mikopo kwa kushirikiana na benki ya Covenant’ alisema Basilla.
IMEDHIBITISHWA
NA:
Basilla Mwanakuzi
No comments:
Post a Comment