Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 19 October 2014

MKULIMA AKUTWA AMECHINJWA


Na Steve William, Muheza
Watu wasiojulikana wamemvamia na kumchinja mkulima wa kijiji cha Mtindiro, Richaridi Saidi, wilayani hapa na kisha kumfungia katika nyumba yake.

 
Akizungumza na NIPASHE, Afisa Mtendaji wa kata ya Mtindiro, Ester Kaima, alisema kuwa mkulima huyo aliuawa na watu hao na kufungiwa ndani ya nyumba yake katika shamba la mmiliki wake Halidi Semboni.
 
Alisema baada ya watu kufanya mauaji hayo walitokomea kusikojulikana.
 
Alisema mwili wa mkulima huyo uligundulika siku ya tatu baadaye baada ya majirani kusikia harufu ikitoka ndani ya nyumba hiyo.
Katika tukio jingine Salima
Rashidi amejiua kwa kunywa sumu.
 
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Kwabada kata ya Mtindiro.
Jeshi la polisi wilayani Muheza limedhibitisha kutokea matukio hayo.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment