Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 11 October 2014

MASHINDANO YA KWAYA YAFANA IRINGA LEO

Kwaya Kuu ya Usharika wa Kihesa ikishiriki mashindano.
Kwaya ya Pomerini. 
Kwaya ya Nyamhanga ambayo ilishika nafasi ya tatu. 
Kweli mwili haujengwi kwa mawe. Baada ya kazi nzito wanakwaya wa Kihesa wakipata chakula. 

Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
Iringa: Kwaya ya Vijana kutoka Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri mjini Iringa imeibuka ya kwanza katika mashindano ya uimbaji yaliyoshirikisha jumla ya kwaya zaidi ya 20.

Mashindano hayo ya Dayosisi ya Iringa, ambayo yalifanyika kwenye Usharika wa Mkwawa mjini humo, yameshuhudia kwaya hizo zikionyesha umahiri katika umbaji wa Note yakiwa na lengo la kuhamasisha uimbaji na kumsifu Mungu.
Aidha, mashindano hayo pia yalishuhudia ushiriki wa mara ya pili wa Kwaya ya Usharika wa Maili Mbili, kutoka mjini Dodoma, ambayo ilionyesha umahiri wa hali ya juu.
Hata hivyo, pamoja na ushindi huo wa Kwaya ya Vijana, bado kwaya zote zilifanya vizuri na kwa hakika kimantiki kila moja imeshinda katika mukhtadha wa kumwimbia Mungu.
Katika orodha hiyo, Vijana ilifuatiwa na kwaya ya Usharika wa Itungi, kwa ya Nyamhanga ikishika nafasi ya tatu na katika nafasi ya nne zilifungana kwaya tatu ambazo ni Ipogolo, Mkimbizi na Dodoma.
Katika nafasi ya tano pia zilifungana kwaya tatu zilizopata alama sawa, ambazo ni Uhominyi, Ipalamwa na Mtwivila.
Kwa Kuu ya Usharika wa Kihesa imeshika nafasi ya sita lakini ikiwa imefungana kwa alama sawa na Ilula na Kilengapasi, wakati kwenye nafasi ya saba kwaya za Balali kutoka Image, Ilula Mtua na Mlandege zilifungana kwa alama sawa huku kwaya za Muhiliwa na Pomerini zikishika nafasi ya nane.
Kwaya nyingine zilizoshiriki ni Mwatasi, Mkwawa, Mbigili, Magulilwa, Ndengisivili na Kipaduka.

No comments:

Post a Comment