Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 6 January 2014

IGP MPYA AKUTANA NA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI


 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu (kushoto) akimfafanulia jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia) kuhusiana na masuala mbalimbali ya uboreshaji wa jeshi hilo. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi na Naibu Inspekta Generali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki. IGP Mangu pamoja na Naibu wake walikutana na Katibu Mkuu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia) akiagana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu baada ya mazungumzo yao kuhusiana na masuala mbalimbali ya uboreshaji wa jeshi hilo. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi na Naibu Inspekta Generali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki. IGP Mangu pamoja na Naibu wake walikutana na Katibu Mkuu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani.

KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment