Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa mauzo wa
kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo
pamoja na ujumbe wake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama kitabu cha picha ya ndege aina ya Boeing 787-8 Dream
liner wakati alipokuwa akisikiliza maelezo yake kutoka kwa Mkurugenzi wa mauzo
wa kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo. Ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba
abiria 262 na itakuwa na uwezo wa kuruka kutoka nchini Marekani hadi Tanzania
bila kutua mahali popote.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mkurugenzi wa mauzo wa Kampuni ya
Ndege ya Boeing Jim Deboo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini
Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Doto James
na anayefuatia ni Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kuhusiana na ununuzi wa ndege
hiyo mpya aina ya Boeing 787-8 Dream liner mara baada ya kumaliza mazungumzo na
Mkurugenzi wa mauzo wa Kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Cuba anayemaliza
muda wake nchini George Luis Lopez Tormo aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Cuba anayemaliza
muda wake hapa nchini George Luis Lopez Tormo aliyefika Ikulu jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya kuaga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Cuba anayemaliza muda
wake hapa nchini George Luis Lopez Tormo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Dkt. Tonia ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) katika Ukanda wa Kusini Mwa Afrika katika Ofisi zake zilizopo Afrika ya
Kusini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia
Kandiero ambaye alifika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo na kuagana na Mhe. Rais
Dkt. Magufuli. Dkt. Tonia ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB) katika Ukanda wa Kusini Mwa Afrika katika Ofisi zake zilizopo
Afrika ya Kusini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mwakilishi Mkazi wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero ambaye alifika Ikulu
kwa ajili ya mazungumzo.Dkt. Tonia Kandiero ameteuliwakuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB) katika Ukanda wa Kusini Mwa Afrika katika Ofisi zake zilizopo
Afrika ya Kusini PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment