Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mh. Jenista Mhagama akiongea na wadau mbalimbali (hawapo pichani) kabla
ya uzinduzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha na
Benjamin Sawe-Maelezo).
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mh. Jenista
Mhagama akizindua Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Kushoto ni Naibu Waziri Mh.
uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Benjamin
Sawe-Maelezo).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mh.
Jenista Mhagama akisoma ujumbe mara baada ya kuzindua Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama akikabidhi Tuzo ya
Ushiriki kwa mmoja wa wadau waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi uliofanyika jijin Dar es Salaam leo. (Picha na Benjamin
Sawe-Maelezo).
Mkurugenzi Mtendaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
Masha Mshomba akiongea na wadau mbalimbali kabla ya uzinduzi wa Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (jana). (Picha na Benjamin
Sawe-Maelezo).
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
Emanuel Humba akiongea na wadau mbalimbali kabla ya uzinduzi wa Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Benjamin
Sawe-Maelezo).
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi wakimsikiliza Waziri wa Kazi, Mh. Jenista Mhagama wakati wa Mfuko
huo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Benjamin
Sawe-Maelezo).
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama (wanne kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika
picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Serikali na zisizo za
Kiserikali baada ya uzinduzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha na
Benjamin Sawe-Maelezo).
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi wakimsikiliza Waziri wa Kazi, Mh. Jenista Mhagama wakati wa Mfuko
huo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Benjamin
Sawe-Maelezo).
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na
Ajira Mh. Antony Mavunde akiongea na wadau mbalimbali (hawapo pichani)
kabla ya uzinduzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha na
Benjamin Sawe-Maelezo).
Na Ismail Ngayonga
MAELEZO - Dar es Salaam
SERIKALI
imewaagiza Waajiri wote nchini kuwasilisha kwa wakati michango ya mafao ya
fidia kwa wafanyakazi ili kuwawezesha watumishi wao kupata huduma za matibabu
pindi watakapoumia au kuugua wakiwa katika maeneo yao ya kazi.
Agizo
hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Ulemavu)
Jenister Mhagama wakati alipokuwa akizindua huduma za utoaji wa mafao ya fidia
na ubia baina ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) na watoa huduma za afya
nchini.
Mhagama
alisema suala la uchangiaji wa mafao hayo sio la hiari ila lipo kisheria na
hivyo ni wajibu wa waajiri wote nchini kuhakikisha kuwa wafanyakazi wao
wanaingizwa katika mfumo huo ili kuwawezesha wafanyakazi kuwa na uhakika wa
kulipwa fidia pindi wanapokuwa kazini.
“Katika
mwaka wa fedha 2016/17 Serikali imelipa michango yote ya wafanyakazi wake, na
huu ni mfano unaopaswa kuigwa na waajiri wengine nchini, na natoa rai kwa Chama
cha Waajiri Nchini (ATE) na Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA)
linasimamia suala hili” alisema Mhagama.
Aidha
Mhagama alisema lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo wa wafanyakazi nchini ni
kusaidia kutatua kilio cha muda mrefu cha wafanyakazi wa sekta za umma na
binafsi, ambao wamekuwa wakilalamikia huduma hafifu zinazotolewa pindi wapatapo
majanga mbalimbali wakiwa kazini ikiwemo ajali na vifo.
Waziri
Mhagama alitaka Bodi ya mfuko huo kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria
zilizopo ili kuhakikisha kuwa waajiri wote hususani wa sekta binafsi
wanawasilisha michango kwa wakati.
Akifafanua
zaidi Waziri Mhagama aliuataka mfuko huo kujitangaza zaidi kwa sekta zisizo
rasmi ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi hususani wa kipato cha chini
kujiunga na mfuko huo na kuwasaidia kufaidi huduma zinazotolewa.
“Natoa
rai kwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii nchini ikiwemo wa WCF mjitangaze katika
sekta zisizo rasmi ikiwemo waendesha bodaboda, akina mama lishe, kwa kuwa idadi
yao ni kubwa na hiyo itawezesha kupata
wanachama wengi zaidi” alisema Mhagama.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Masha Musomba alisema hadi kufikia
sasa mfuko huo umeweza kutoa usajili wa waajiri
5945 pamoja na kuendesha mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo watumishi wa
mfuko huo ikiwemo madaktari.
Aidha
Musomba anasema pia mfuko huo umeingia ubia na taasisi 7 za utoaji huduma za
afya nchini, ambazo ni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Taasisi ya Mifupa
Muhimbili (MOI), na Taasisi ya Kansa ya Ocean Road.
Musomba
anazitaja taasisi nyingine kuwa ni Strategis, AAR, mfuko wa Jubilee, na
Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo taasisi hizo zinazoendelea kushughulikia
kesi 189 zilizolipotiwa katika mfuko huo.
Naye
Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE), Aggrey Mwinuka alisema mfumo
huo wa fidia umekuja katika wakati muafaka kwa kuwa sheria zilikuwepo katika
vitabu na hazikuwa na utekelezaji uliokusudiwa.
Mwinuka
alisema ili kuhakikisha kuwa malengo ya mfuko huo yanatekezeka ni wajibu wa
Serikali kuhakikisha kuwa inafanya majadiliano ya mara kwa mara na waajiri ili
kuangalia viwango vya makato ya michango ya wafanyakazi wa sekta ya umma na
binafsi.
Mwenyekiti
wa Bodi ya mfuko huo, Emmanuel Homba alisema uwekaji wa mfumo wa mafao ya fidia
utawezesha wafanyakazi katika sekta za
umma na binafsi kuchangia kikamilifu katika Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano
ya ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.
No comments:
Post a Comment