Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya
Kuambukiza kwenye viwanja vya Leaders Club.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza ambapo aliwaambia wananchi walishiriki kwenye tukio hilo kuwa siri kubwa ya mafanikio yake ya kuonekana yupo imara ni mazoezi hivyo aliwataka wananchi wajenge tabia ya kushiriki na kufanya mazoezi kwani kutawaepusha na maradhi mengi .
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim akihutubia kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua rasmi Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza
matembezi ikiwa sehemu ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi akiongozana na Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaji Ali
Hassan Mwinyi (kushoto) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalim kabla ya kufungua Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti
Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza kwenye viwanja vya Leaders Club viongozi
wengine walioshiriki matembezi hayo ni pamoja na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalah, Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda .
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kufungua wa Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya
Kuambukiza kwenye viwanja vya Leaders Club.
....................................................................................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa muda wa
miezi mitatu kwa Halmashauri zote nchini kurudisha serikalini haraka maeneo ya
michezo yaliyovamiwa na watu kwa ajili ya kufanya shughuli zao binafsi.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo baada ya kushiriki matembezi na
kuzindua wa kampeni ya Kitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
kwenye viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Makamu wa
Rais ameonya kuwa kama watendaji wa mikoa na halmashauri watashindwa kurudisha
maeneo hayo basi watenge haraka maeneo mengine kwa ajili ya wananchi kufanya
mazoezi kama hatua ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Katika
kuunga mkono utaratibu wa kufanya mazoezi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi wa mikoa na wilaya zote kuweka
utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa mwezi mara Moja.
“Nitamke
kuwa kila Jumamosi ya pili ya mwezi itakuwa siku ya mazoezi kwa afya kwa sababu
mazoezi ni afya na nawaasa wananchi kufanya mazoezi na kuanzisha na kujiunga na
vikundi vya mazoezi na serikali itatimiza wajibu wake wa kuweka mazingira
mazuri ya kufanyia mazoezi kote nchini”
Makamu wa
Rais pia ameagiza watendaji wa Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia kurudisha
mchakamchaka mashuleni kulingana na maeneo yalivyo.
Amesema
mchakamchaka utasaidia kuimarisha afya za wanafunzi na kukabiliana na magonjwa
mbalimbali.
“Natoa
rai utaratibu wa mchakamchaka katika shule zetu urudishwe mara Moja katika Muda
ambao utaonekana ni mwafaka kwa shule husika”.
Katika
hatua nyingine, Makamu
wa Rais ameiagiza Wizara ya Afya kukamilisha haraka mchakato wa kuunda kamati
ya kushughulikia magonjwa yasiyo ya kuambukiza itakayojumuisha wadau kutoka
wizara mbalimbali nchini.
Amesisitiza
kuwa mchakato huo ni lazima ukamilike tarehe 1 machi mwaka 2017.
Kwa
upande wake, Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema
magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamekuwa yanaongezeka sana duniani kote hasa kwenye
nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania ambapo magonjwa hayo
mpaka sasa yanachangia asilimia 27 ya vifo Duniani.
Amesema
utafiti uliofanyika mwaka 2012 uliohusisha wilaya 53 hapa nchini umeonyesha
viashiria hatarishi vya magonjwa hayo ambapo asilimia 26 ya wananchi ni wanene
kupita kiasi,asilimia 26 wana lehemu nyingi mwilini na asilimia 25.9
wanashinikizo kubwa la damu.
Utafiti
huo pia ulionyesha kuwa asilimia 15.9 ya wananchi wanavuta sigara na asilimia
97.2 ya wananchi wanakula mboga mboga na matunda chini ya mara tano kwa siku.
Waziri wa
afya Ummy Mwalimu amesema watanzania wanaweza kukabiliana na magonjwa hayo kwa
kufanya mazoezi ya viungo angalau mara tatu kwa wiki kwa muda wa nusu saa,
kuzingatia ulaji wa vyakula unaofaa,kupunguza matumizi ya pombe kupita kiasi na
kujiepusha na matumizi ya tumbaku.
Kwa
upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi katika nasaha
zake amewahimiza Watanzania kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya zao.
Amesema
kama watanzania watafanya mazoezi wataepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza
ikiwemo ugonjwa wa moyo,kisukari,uti wa mgongo na mifumo ya neva na figo.
No comments:
Post a Comment