Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (kushoto) akiwa katika Banda la Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakati wa kufunga Maonesho ya viwanda viwanja vya sabasaba
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa mfuko wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe akitoa maelezo mbalimbali juu ya Mfuko huo.
Kulia Afisa Mwendeshaji Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji
Jamadary akitoa elimu kwa Mwananchi kuhusiana na uchangiaji wa hiari huku
akimwonyesha bango lililo orodhesha mafao yanayo tolewa na PSPF kupitia PSS.
Wananchi mbalimbali wakiwa wametembelea banda la mfuko wa
pensheni wa PSPF kwaajiri ya kujifunza shughuli zinazofanywa na mfuko huo.
Mmoja wa wananchi walio fika na kujisajiri na mfuko wa PSPF
akijaza fomu ya kujiunga na mpango wa uachangiaji wa hiari (PSS).
Afisa Mwendeshaji Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary
akikabidhi vitambulisho kwa badhi ya wanachama walio jiunga na mpango wa
uchangiaji kwa hiari katika maadhimisho ya maonyesho ya viwanada jijini dar
Afisa Mwendeshaji Mfuko wa Pensheni wa PSPF Asmahan haji
akiendelea kufanya shughuli za kiofisi katika banda la PSPF ndani ya maonyesho
ya viwanda (saba saba) jijini Dar es salaam.
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa mfuko wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe (Kushoto), akiwapa vitambulisho wanachama waliojiunga na mfuko huo kupitia uchangiaji wa hiali (PSS)
Mfuko wa Pensheni wa PSPF wahitimisha maonyesho ya viwanda
vidogovidogo na wajasiliamali kwa kugawa vitambulisho kwa watu walio jiunga
na mfuko huo katika uwanja wa maonyesho ya biashara waMwl.J.K Nyerere (saba
saba) jijini Dar es salaam ,maonyesho hayo yaliyodumu kwa takribani siku tano
ambapo yalianza Tareh 5.12.2016 na kuhitimishwa
Tarehe 11 /12/2016 yakiwa na kauli mbiu isemayo ‘TANZANIA SASA TUNAJENGA
VIWANDA’ PSPF walikuwa sambamba katika maonyesho hayo ili kuwaelimisha na
kuwasihi wajasiliamali kujiunga na mfuko huo na kuweza kuwaeleza faida pindi watakapo jiunga.
Mgeni rasmi aliye hitimisha maonyesho hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru alipata
fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ambapo alitembelea banda la PSPF na
kuona namnagani wanavyo fanya kazi huku akisifia Mfuko huo kwa kuweza kuanzisha
mafao mbalimbali ambayo yanawaokoa wajasiliamali mbalimbali kwa kupata mitaji
inayoweza kuwasaidia katika shughuli za kila siku.
Mfuko wa Pesheni wa PSPF ambao unatoa mafao mbalimbali
katika jamii likiwemo fao la ujasiliamali, elimu ,uzee ,kifo na mengine mengi
umeweza kuendeleza elimu kwa wananchi ili waweze kujiunga na mfuko na kunufaika
kwa kutokana na mafao yaliyopo ambapo mtu yeyote anauwezo wa kumudu kwani
kupitia mpango wa uchangiaji kw hiari (PSS)
ambao unamwezesha Mwananchi yeyote kuchangia na kunufaika na mafao hayo
.
Aidha Afisa Mwendeshaji wa PSPF katika mpango wa uchangiaji
wa hiari PSS Haji Jamadary aliweza
kuwaelemisha wananchi mbalimbali walioweza kutembelea banda la PSPF katika
maonyesho hayo na kufanikiwa kujiunga na mpango huo wa hiari alisema
“pindi unapo kuja
kujinga na PSS moja kwa moja unakuwa mwanafamiliya Ya PSPF kwani Dhumuni letu
ni kukufikia na kukupa huduma zilizo bora na zitakazo kuwa na dhamana katika
maisha ya kila mmoja ambapo mwanachama ataweza kunufaika kwa kupata njia ya
matibabu kupitia shirika la bima ya afya la taifa NHIF kwani wametia nguvu PSPF
ili waweze kuhudumia jamii kwa ujumla Na Kwaharaka zaidi “
No comments:
Post a Comment