Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Chama Cha
Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania ambao walimtembelea ofisini
kwake leo.
.............................................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewakaribisha
wawekezaji kutoka nchini China kuja kuwekeza nchini katika maeneo mbalimbali
ikiwemo uvuvi katika bahari,madini, utalii, ujenzi wa viwanda na miundombinu.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na kufanya
mazungumzo na Watendaji Wakuu wa makampuni makubwa kutoka nchini China ambao
walikuja hapa nchini kutafuta fursa za uwekezaji.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wawekezaji hao kuwa Tanzania ni nchi
salama kwa ajili ya kuwekeza kutokana na amani iliyopo na kwa sasa Serikali
inaendelea na mkakati kuondoa vikwanzo vinavyokwamisha uwekezaji ikiwemo
ukiritimba na rushwa nchini.
Amesema
Tanzania na China zinamahusiano mazuri na ya muda mrefu hivyo ni muhimu
mahusiano hayo yakaendelea kuimarishwa zaidi kama hatua ya kukuza biashara kati
ya nchi hizo mbili kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa Tanzania na China.
Amesisitiza
muhimu wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya Chama cha Wafanya Biashara wenye
Viwanda na Wakulima nchini (TCCIA) na Chama cha Wafanya biashara kutoka
China kama hatua ya kuimarisha kwa angalia fursa bora za uwekezaji kati ya
China na Tanzania.
Makamu wa
Rais pia ameishukuru nchi ya China kwa kuichangua Tanzania kuwa miongoni mwa
nchi Nne za bara la Afrika kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda.
Kwa
upande wao, Watendaji hao wa makampuni makubwa kutoka nchini China wamesema kwa
sasa wapo mbioni kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza vifaa tiba katika eneo
la Mbagala jijini Dar es Salaam na wameshapewa ekari 160 kwa ajili ya kujenga
kiwanda hicho.
Watendaji
hao wameiomba serikali ya Tanzania isaidie kuhakikisha pindi mradi huo
utakapoanza kujengwa huduma za msingi ikiwemo umeme na maji zinapatikana kwa
urahisi kwenye eneo hilo.
No comments:
Post a Comment