Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
na Balozi wa Kenya Nchi Mhe. Ali Makwere, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
na Balozi wa Brazil Nchi Mhe. Carlos Alfonso Puente, Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
na Balozi wa Denmark Nchi Mhe. E. Hebogand Jensen, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
kwenye picha ya pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa
Mataifa (UNICEF), Mhe. Maniza Zaman, mara baada ya kumaliza mazungumzo,Ikulu
jijini Dar es Salaam.
.................................................................
Mabalozi wa
Nchi Mbili za Brazil na Kenya wameipongeza serikali ya awamu ya Tano kwa
mipango na mikakati yake ya madhubuti ya kulifufua Shirika la Ndege Tanzania -ATCL
– kwa kununua ndege mpya kama hatua ya kuhakikisha shirika hilo linakuwa bora
katika utoaji wa huduma za usafiri wa anga ndani na nje ya nchini.
Mabalozi hao
wamesema hatua hiyo ya kuliimarisha Shirika la Ndege la Tanzania itasaidia kukuza shughuli za utalii na pato la
taifa kwa ujumla.
Balozi wa
Brazil nchini Carlos Alfonso Puente na Balozi wa Kenya hapa nchini Chirau Ali
Makwere wametoa pongezi hizo mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan ikulu jijini Dar es salaama.
Kwa upande
wake, Balozi wa Brazil nchini Carlos Alfonso Puente amesema kutokana na nchi
hiyo kuwa ni miongoni mwa nchi kadhaa Dunia zenye viwanda wa kutengeneza ndege hivyo
serikali ya Tanzania ina nafasi nzuri ya kununua ndege nchini Brazil hasa kulingana
na mahusiano mazuri na ya muda mrefu yaliyopo kati ya nchi hizo mbili.
Kufutia wito
huo wa Balozi wa Brazil Nchini, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wa nchi
ya Brazil kuja nchini kutangaza bidhaa wanazotengeneza hasa ndege kama hatua ya
kuimarisha mahusiano ya biashara kati ya Brazil na Tanzania.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kutokana na nchi ya Brazil kupiga hatua
kubwa katika uzalishaji wa sukari na Tanzania ni moja ya nchi yenye maeneo mazuri kwa ajili ya uwekezaji huo hivyo
ni muhimu kwa wafanyabiasha wa Brazil kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika
sekta hiyo.
Kuhusu
kilimo cha Pamba nchini, Balozi wa Brazil Carlos Alfonso Puente amesema
serikali ya nchi hiyo imeanzisha mradi kabambe unaolenga kusaidia uzalishaji
bora wa pamba katika mikoa ya kanda ya ziwa mradi ambao utagharimu dola za Kimarekani
milioni Sita kwa miaka minne nchini.
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
katika mazungumzo yake na Balozi wa Kenya hapa nchini Chirau Ali Makwere
amesisitiza kudumishwa na kuendelezwa kwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya
Tanzania na Kenya hasa katika uimarishaji wa biashara na uwekezaji kati ya nchi
hizo Mbili.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito maalum kwa Watanzania kuchangamkia fursa
ya kufanya biashara na nchi ya Kenya kutokana na nchi mbili kuwa na mahusiano
mazuri ya kibiashara.
Wakati huo huo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini Hebogand Jensen ambaye
amemweleza Makamu wa Rais nia ya nchi hiyo kwa ushirikiano na nchi nyingine ya
kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea wilayani Kilwa.
Balozi huyo
wa Denmark nchini amesema anaimani kiwanda hicho kitakachojengwa nchini
kitafanya uzalishaji mkubwa na kutoa ajira kwa mamia ya wananchi wa Tanzania.
Kwa upande
wake, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali katika kuelekea
kwenye uchumi wa viwanda imeweka mazingira mazuri kwa ajili ya wawekezaji
wanaotaka kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini kama hatua ya kukuza
uchumi wa nchi.
No comments:
Post a Comment