WAKATI ‘raundi ya 17 ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ikitaraji kuendelea jumamosi hii,kikosi cha Mbeya City fc kieendelea na mazoezi ikiwa ni matayarisho ya mchezo namba 130 dhidi ya wageni Toto Africans ya Mwanza uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa.
Kwenye mazoezi ya timu hiyo leo asubuhi, Ofisa habari wa kikosi hicho Dismas Ten amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri na wachezaji wote wakiwa na ari kubwa licha ya kuwepo kwa taarifa za majeraha kwa mlinzi Haruna Shamte aliyeumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar.
Akiendelea zaidi Ten aliweka wazi kuwa kwenye mchezo huo dhidi ya Toto, City inaweza kukosa huduma ya mlinzi wake Haruna Shamte aliyepata majeraha ya kifundo cha mguu kwenye mchezo uliopita ingawa jopo la madaktari wameahidi kutoa taarifa mpya juu yake siku ya kesho huku akigusia pia suala la ITC ya kiungo Mrisho Ngassa.Kama unavyofahamu jumamosi iliyopita tulipata suluhu ya 0-0 na Kagera Sugar, mara hii tunafanya maandalizi makubwa kuhakiksha tunashinda mchezo ujao, pointi tatu ni jambo pekee linalohitajika kwenye duru hii ya pili, tunaifahamu Toto kuwa ni timu nzuri lakini mara kadhaa sisi tumekuwa tunaibuka wababe dhidi yao, alisema
No comments:
Post a Comment