Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wakati ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya
Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam.

Salaam ambapo aliwapongeza TAFOPA kwa kazi nzuri wanayoifanya lakini pia aliwataka Wasindikaji kuongeza ushirikiano ili kufikia maendeleo na mafanikio ya juu.
Wadau waliohudhuria na kushiriki wakimsikiliza kwa makini Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wakati ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya
Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa TAFOPA Bi. Suzy Laizer akihutubia
wakati ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya
Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam, mgeni rasmi kwenye mkutano huu alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia
bidhaa mbalimbali za vyakula vilivyosindikwa zinazotengenezwa na
wajasiriamali muda mfupi kabla ya kufungua wa mkutano wa Wadau wa
kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye
ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali
ipo mbioni kupunguza muda wa utoaji wa leseni za biashara nchini ili kutoa
fursa kwa wananchi wengi zaidi kupata leseni hizo kwa ajili ya shughuli za
kibiashara.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam katika ukumbi
wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati anafungua mkutano wa
wadau wa kuendeleza maeneo tengefu ya viwanda vya usindikaji wa vyakula nchini.
Makamu wa
Rais amesema mpango utaenda pamoja na kupunguza baadhi ya kodi na tozo ambazo
ni kero kwa wananchi hasa wenye viwanda kama hatua ya kukuza biashara na
uwekezaji katika sekta ya viwanda nchini.
Amesisitiza
kuwa Serikali inaendelea na mazungumzo na wenye mabenki hususani benki ya TIB
ili kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda.
Kuhusu
usindikaji wa bidhaa nchini, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni
Mjumbe katika jopo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kumuwezesha mwanamke
kiuchumi akiwakilisha nchi za ukanda wa Kusini na Mashariki mwa Afrika
amepongeza jitihada zinazofanywa na wasindikaji wadogo nchini katika
utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ambazo zitakidhi katika masoko ya ndani na
nje ya nchi.
“Serikali inafarijika sana kuona kuwa wasindikaji wadogo nchini
wamethubutu na wana uwezo wa ushindani katika biashara ya ndani na hata nje,
hivyo tunayohaki ya kujigamba kwa kuthubutu, Tumeweza na Tuendelea Kusonga mbele”
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan amesema umefika wakati kwa Wizara na taasisi za Serikali na wadau
wa maendeleo kuona umuhimu wa kuhakikisha viwanda vinajengwa vijijini ili
mkulima mdogo anapolima awe na uhakika wa kupata soko katika viwanda hivyo.
Amesema kuwa hali hiyo itaondoa changamoto ya kusafirisha bidhaa
nyingi ambazo zinaharibika njiani au zinapofika sokoni na hivyo kukosesha jamii
kipato kilichotarajiwa.
Makamu wa Rais pia amehimiza watafiti nchini wajielekeza
katika kufanya tafiti ambazo zitasaidia sekta binafsi na serikali kwa ujumla kuhusu
namna bora ya kukuza sekta ya viwanda nchini.
No comments:
Post a Comment