Ligi ya vijana kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea katika vituo viwili vya Kagera na Dar Es Salaam ambapo duru la kwanza linatarajiwa kumalizika Desemba 05, 2016.
Katika kituo cha Dar es Salaam, Simba ya Dar es Salaam inatarajiwa kucheza kesho Jumapili Novemba 4, 2016 na JKT Ruvu ya Pwani katika mchezo utakaoanza saa 8.00 mchana wakati saa 10.30 kutakuwa na mchezo kati ya Tanzania Prisons ya Mbeya na Ndanda FC ya Mtwara.
Kesho hiyo hiyo, Desemba 4, mwaka huu katika kituo cha Kagera kutakuwa na mchezo kati Stand United ya Shinyanga itakayocheza na Young Africans saa 8.00 mchana wakati ya Mwadui pia ya Shinyanga itacheza na Mbao saa 10.30 jioni.
Jumatatu Desemba 5, mwaka huu ratiba itakamilika katika kituo hicho cha Kagera kwa Kagera Sugar kucheza na African Lyon ya Dar es Salaam saa 8.00 mchana wakati Azam FC ya Dar es Salaam na Toto Africans ya Mwanza zitamaliza saa 10.30 jioni.
Kwa siku hiyo ya Jumatatu, Kituo cha Dar es Salaam pia kutakuwa na mechi mbili ambako Majimaji ya Songea itacheza na Ruvu Shooting ya Pwani saa 8.00 mchana wakati Mtibwa Sugar ya Morogoro itacheza na Mbeya City ya Mbeya saa 10.30 jioni.
Baada ya kumalizika kila kundi litatoa washindi wawili watakaocheza nusu fainali na baadaye fainali.
Hatua ya nusu fainali itachezwa jijini Dar Es Salaam katika uwanja wa Azam Complex tarehe 09.12.2016 wakati fainali itachezwa tarehe 11.12.2016 katika uwanja huo huo.
No comments:
Post a Comment