Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 20 October 2014

UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO: UKAGUZI WA BARABARA YA TUNDUMA - SUMBAWANGA


Kaimu Meneja wa wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Masuka Nkina (wa kwanza kulia mwenye shati jeupe) akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa mizani ya Nkangamo katika barabara ya Tunduma – Laela- Sumbawanga. Utendaji wa mizani hiyo ni kwa kutumia kompyuta ambapo mteja anachapishiwa risiti yake hapo hapo inayoonyesha taarifa zake zote. Kama mzigo utakuwa umezidi pia risiti hiyo itaonyesha faini anayotakiwa kulia.

Mhandisi Happiness Mgalula, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Miundombinu na Huduma  akifafanua jambo wakati wa ukaguzi wa barabara ya Tunduma – Sumbawanga . Mhandisi Mgalula anaongoza timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo  kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Mhandisi Julius Isoka ambaye ni Mhandisi Mshauri wa Barabara ya  Tunduma- Sumbawanga kutoka kampuni ya Nicholous Odweyer akiwaelezea timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambao wanatembelea barabara hiyo jinsi ambavyo daraja linasukwa kutoka chini mpaka juu.  Barabara hii inajengwa kwa ufadhili wa Watu wa Marekani chini ya Mradi wa Millenium Challenge (MCC).
Daraja la Kashahanzi moja ya daraja kubwa na linalojengwa kwa umahiri mkubwa katika barabara ya Tunduma  –Sumbawanga.  
PICHA ZOTE NA JOYCE MKINGA

No comments:

Post a Comment