Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 25 October 2014

SERENGETI FIESTA NDANI YA KIGOMA LEO

Mr Blue atafanya vitu vyake ndani ya Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma

Shoo ya tamasha la Serengeti Fiesta 2014 limeelekea Kigoma leo tarehe Oktoba 25, baada ya kuburudisha vilivyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo zaidi ya mashabiki 50,000 walihudhuria katika tamasha hilo.

Tamasha la Serengeti Fiesta limeingia mjini Kigoma, kama sehemu ya kuwapa zawadi  mashabiki wake kutokana na mafanikio makubwa waliyowahi kuyapata mkoani humo. Shoo hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa mkoa huo imepangwa kufanyika katika uwanja wa Lake Tangayika ambapo wakazi wa mji huo wanahamu kubwa ya kuona wasanii  nyota wakituimbuiza kwa mara ya kwanza katika mkoa huo.    
Kwa mujibu wa taarifa toka kiwanda cha bia cha Serengeti kupitia kinywaji chake cha Serengeti Premium Lager ambao ndio wafadhili wakuu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2014 wameitaja shoo ya Kigoma kama ya 17 katika ziara zao za mikoani. 
Rugambo Meneja chapa wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi na alinaahidi kwamba shoo  itakuwa moja kati ya shoo bora kabisa, aliwataja wanamuziki wa nchini watakaotuimbiza katika shoo hiyo itakayofanyika katika viwanja vya Lake Tanganyika.
Baadhi ya waliodhibitisha kufanya shoo hiyo ni pamoja na Ali Kiba, Stamina, Ney wa Mitego, Linah, Recho, Young Killa, Christian Bella, Mwasiti, Dully Sykes, Mo Music, Baraka Da Prince, Supa Nyotas:- (G-Luck, K-Style and Edo boy)”.

No comments:

Post a Comment