Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limetumia jumla ya shilingi
milioni 731,360,000/= kusaidia miradi ya vijana ya kufyatua tofali nchini.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Mawasiliano
wa NHC, Bi Suzan Omari wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Vijana kilichofanyika hivi
karibuni mkoani Tabora.
Bibi Suzan amefafanua kuwa fedha hizo zinahusisha ununuzi wa mashine uliyogharimu
shilingi 297,000,000/=, mafunzo ya wakufunzi yaliyogharimu shilingi
47,000,000/= na uwezeshaji mtaji wa
kuanzia kazi za vikundi vya vijana kufyatua matofali shilingi 81,500,000/=.
Ameongeza kuwa matumizi mengine kuwa ni usambazaji
wa mashine uliyogharimu shilingi 30,000,000/=, uhakiki wa ubora wa mashine
uliofanywa na wataalamu kutoka VETA shilingi 6,400,000/=, fedha za kununulia
vifaa vya mafunzo katika kila halmashauri vilivyogharimu shilingi 130,400,000
na posho ya wakufunzi wa VETA ni shilingi 139,060,000/=.
Bi Suzan amewataka vijana kote nchini kutumia fursa
hii kwa ajli ya maendeleo yao ikiwemo na kuondokana na tatizo la kukukosa
ajira. Amayetaka mashirka mengine nchini kuiga mfano wa NHC ili kunusuru nguvu
kazi hii kubwa.
Kwa upande mwingine, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC,
Bw, Muungano Saguya amesema kuwa wadau zikiwemo Halmashauri, Maafisa Vijana wa
Mikoa na wilaya kwa kushirkiiana na mamameneja wa mikoa wa NHC wathamini mradi
huu kwa kufuatilia ufanisi wake ili mradi huo uwe endelevu.
Ameongeza kuwa mradiukiwa endelevuna kusaidia
kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, bajeti itaongezeka kwa mwaka wa fedhaujao
ilikusaidia zaidi mradi huo kwa vijana.
Naye Meneja
wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Tabora, Bw. Erasto Chilambo amesema
maafisa vijana wawaunganishe vijana katik a vikundi ili watumie fursa hii
kujiendeleza na kuacha kubweteka na kulalamika kwa kukosa ajira.
Aliongeza kuwa vijana wasiwe sehemu ya tatizo la ajira bali
wawe watatuzi wa changamoto inayowakabili
ya kukosa ajira.
Kikao hiki ni kikao cha kuwakumbusha maafisa vijana
majukumu yao kuwasaidia kupata uzoefu
toka kwa wenzao. Kimeandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo.
No comments:
Post a Comment