Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 19 October 2014

KIKUNDI CHA WANAWAKE CHA ATUE CHATEMBELEA WAGONJWA HOSPITALI YA MKOA IRINGA

 "...Nilipokuwa mgonjwa hukuja kuniangalia..." Naam, kuwatembelea wagonjwa ni ishara ya upendo unaohubiriwa na Maandiko Matakatifu. Wanawake wa kikundi cha ATUE cha mjini Iringa wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Asasi hiyo Bibi Emery Kiwanga akitoa maelezo kabla ya kuaingia wadini leo hii katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa. Picha zote na Angel Kiria wa Brother Danny Blog.

 Baadhi ya vitu ambavyo wanawake wa kikundi cha ATUE walikwenda kuwapatia wagonjwa wakati walipowatembelea katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa leo hii.
 Bibi Emery Kiwanga akionyesha baadhi ya zawadi walizokwenda nazo kwa ajili ya kuwapatia wagonjwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Iringa leo hii.
 Wanachama wa kikundi cha wanawake cha ATUE wakiwa nje ya Hospitali ya Mkoa wa Iringa tayari kuwatembelea na kuwajulia hali wagonjwa.
 Hapa ni ndani ya wadi ya akinamama.
 Na hapa ni ndani ya wadi ya watoto.
 Mtoto ambaye hakujulikana mara moja jina lake akionyesha uso wa matumaini huku mama yake akijiandaa kumpatia uji.
 Mchungaji Fwemi akimfariji mama mtoto ndani ya wadi hiyo ya watoto katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa.
 Mmoja wa wagonjwa katika hospitali ya Mkoa wa Iringa akitazama sukari aliyopewa.
 Muuguzi katika wadi ya akinamama akitoa maelezo.
 Mmoja wa wagonjwa katika wadi ya watu wenye matatizo ya akili akiwa amejipumzisha.
Mwenyekiti wa asasi ya ATUE, Bibi Emery Kiwanga, akizungumza na wanachama wa kikundi hicho mara baada ya kutembelea wadini.

No comments:

Post a Comment