Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 2 January 2014

SAMWEL SITTA AENDELEA 'KULIA' NA MAFISADI

Samuel Sitta akiwa na Rostam Aziz

Na Waandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta amesema vijana watafanya makosa endapo tu wataikabidhi nchi mikononi mwa wahuni ambao wanapenda kutumikia matumbo yao kwa nguvu ya pesa kitu kitakachowacheleweshea maendeleo yao.
Sitta anayetajwa kuwa miongoni mwa wawania urais 2015, aliyasema hayo juzi usiku kwenye mkesha wa Mwaka Mpya uliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo alikuwa akimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete.
“Mtafanya makosa kuwapa nchi watu wa jinsi hii ambao badala ya kuwatumikia wananchi wenye hali ngumu  kila kukicha, wanazidi kuteseka kunakosababishwa na mafisadi wachache.
“Endapo vijana wataendelea kupima viongozi kwa nguvu na uwezo wa pesa, tutaendelea kuchelewesha maendeleo ya nchi,” alisema Sitta.
Mbali na hayo, Waziri Sitta alibainisha kuwa kuna baadhi ya viongozi yeye akiwa mmojawao wanaweza kuibadilisha nchi, kwani maono yao ni kufuata tochi ya Mwalimu Julius Nyerere.
Mkesha huo ulioandaliwa na Umoja wa Makanisa Tanzania, ulihudhuriwa viongozi mbalimbali wa Serikali na mabalozi.

CHANZO: Mwananchi

No comments:

Post a Comment