Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 2 January 2014

NDOA SABA ZAFUNGWA KWA MPIGO IBADA YA MWAKA MPYA


Na Flora Mwakasala 

NDOA saba zimebarikiwa katika ibada ya Mwaka mpya, iliyofanyika katika Kanisa la la Anglikana la Mtakatifu Yohana Mbatizaji Minyonyoni, Kigogo Luhanga, jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Thomas Mwayela wa kanisa hilo, alibariki ndoa hizo jana katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya kumaliza mwaka 2013 na kuingia mwaka 2014.
Akibariki ndoa hizo, Mchungaji Mwayela aliwataka waumini hao waishi maisha ya kumpendeza Kristo, wasamehe na kusahau yote yaliyopita bali waanze kuhesabu jana ndiyo siku yao ya kwanza katika ndoa.
Akizungumza na gazeti hili, Katibu Msaidizi wa Kamati ya Mawasiliano na Mahusiano, Steven Masimba alisema wameamua kubariki ndoa za watu hao, kwa kuwa ni Wiki ya Familia Takatifu na wanapenda watu waanze mwaka huku familia zao zikiwa zimekamilika kiimani.
Alisema watu wengi walikuwa wanaishi kama mume na mke kabla ya kufunga ndoa na katika kuhakikisha mambo ya kiimani yanakaa vizuri katika kanisa lao, wakawashauri wabariki ndoa zao.
Alisema lengo ni kuhamasisha watu wengine ambao wanaishi bila kufunga ndoa wabariki ndoa zao na kuishi maisha yanayompendeza Kristo.
“Kubariki ndoa ndiyo msingi wa Kristo kwasababu kuishi bila kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maagizo ya Kristo na kama kanisa tunawasaidia kwa kuwarejesha kw ukristo kamili na ndoa timilifu,” alisema.
Katika ibada hiyo, pia waliombea watoto yatima, na kuwatia moyo wajane na wagane waendelee kuishi maisha yanayompendeza Mungu pia waliombea vijana.

CHANZO: Habarileo

No comments:

Post a Comment