Ikiwa na ari, nguvu na kujaa hamasa na matumaini ya kushinda, timu ya mpira wa miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, kesho Jumamosi Agosti 6, 2016 itaingia Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Magharibi mwa Mji wa Johannesburg, Afrika Kusini kucheza na wenyeji katika mchezo wa awali kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, zitakazofanyika Madagascar hapo mwakani.
“Tutaifunga Afrika Kusini hapa kwao,” ni maneno ya Mchawi Mweusi - Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, alipozungumzia mchezo huo utakaoanza saa 9.00 alasiri kwa saa za Afrika Kusini wakati huko Tanzania itakuwa ni saa 10.00 jioni katika uwanja ambao hutumiwa na timu ya Moroka Swallows ambayo kwa sasa imeshuka daraja hadi la pili.
Afrika Kusini ambayo Serengeti Boys inacheza nayo leo ni mtihani wa kwanza kati ya miwili kabla ya kutinga Madagacar. Mchezo wa kwanza unafanyika hapa Afrika Kusini, kabla ya kurudiana Agosti 21, 2016 kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi-nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na Mchawi Mweusi ambaye jina lake halisi ni Bakari Nyundo Shime, amesema: “Kwa jinsi tulivyojiandaa. Sina wasiwasi na timu yangu.”
Shime amesisistiza: “Najua Afrika Kusini watataka kutumbia mbinu za nyumbani. Lakini sina wasiwasi. Nimelenga kushinda michezo yote iliyo mbele yangu. Si kwamba napigania kufuzu kwenda Madagascar tu kwenye fainali za Afrika, la hasha, nataka timu hii niipeleke Kombe la Dunia.”
Shime ambaye alianza na timu hiyo mwaka mmoja uliopita, amerudia maneno yake: “Sioni kama itakuwa kikwazo kuifanikisha kufika fainali za Kombe la Dunia. Namuomba Mungu atunyooshee mkono wake, nawaombea viongozi wa TFF wazidi kuihudumia timu hii, lakini pia wadau wengine waisapoti timu hii bila kuangalia au kuchagua mtu anayeongoza TFF. Hii ni timu ya Watanzania wote.”
Shime alishukuru mipango na ahadi ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kugharamia kambi ya siku 10 iliyoyofanyika Madagascar akisema: “Ilikuwsa ni kambi bora. Kwa sasa kikosi changu kinahitaji kulipam deni la Watanzania na ahadi ya Rais Malinzi.”
Kikosi tarajiwa kesho ni Ramadhani Awm Kabwili atakayecheza golini, Kibwana Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage, Vitalis Nkosi, Dickson Nickson Job, Shaban Zuberi Ada, Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali, Mohammed Abdallah Rashid Ibrahim Abdallah Ali na Syprian Benedictor Mtesigwa.
Ili kufika hapo, Serengeti iliifunga Shelisheli jumla ya mabao 9-0 katika mechi mbili za Tanzania na Shelisheli.
Hivi karibuni Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki. Ilishika nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na Marekani.
HAWA NDIO NYOTA WA SERENGETI GUMZO AFRIKA
Jina Kamili: Ramadhan Awam Kabwili
Terehe ya Kuzaliwa: Desemba 11, 2000
Mkoa anakotoka0: Dar es Salaam
Nafasi Anayocheza: Kipa
Jezi Namba: 1
Maoni: Tutafanikiwa
Jina Kamili: Samwel Edward Brazio
Terehe ya Kuzaliwa: Juni 28, 2000
Mkoa anakotoka: Tanga
Nafasi Anayocheza: Kipa
Jezi Namba: 18
Maoni: Kucheza Fainali za Kombe la Dunia vijana
Jina Kamili: Kelvin Deogratias Kayego
Terehe ya Kuzaliwa: Juni 5, 2001
Mkoa anakotoka: Geita
Nafasi Anayocheza: Kipa
Jezi Namba: 30
Maoni: Ahsate TFF, ahsante Jamal Malinzi na viongozi wote, ahsante makocha
Jina Kamili: Kibwana Ally Shomari
Terehe ya Kuzaliwa: Januari 1, 2000
Mkoa anakotoka: Morogoro
Nafasi Anayocheza: Beki wa pembeni
Jezi Namba: 12
Maoni: Tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu tufike mbali.
Jina Kamili: Nickson Clement Kibabage
Terehe ya Kuzaliwa: Oktoba 12, 2000
Mkoa anakotoka: Morogoro
Nafasi Anayocheza: Beki wa pembeni
Jezi Namba: 3
Maoni: Nina ndoto kubwa za kuifanyia nchi yangu, ili kufanikiwa lazima tushinde mitihani hii.
Jina Kamili: Israel Patrick Mwenda
Terehe ya Kuzaliwa: Machi 10, 2000
Mkoa anakotoka: Mwanza
Nafasi Anayocheza: Beki wa Pembeni
Jezi Namba: 16
Maoni: Ushindi lazima, ndoto zangu za kucheza soka la kimataifa linaanzia Serengeti na TFF hii ya sasa.
Jina Kamili: Dickson Nickson Job
Terehe ya Kuzaliwa: Desemba 29, 2000
Mkoa anakotoka: Morogoro
Nafasi Anayocheza: Beki wa Kati-Sentahafu
Jezi Namba: 5
Maoni: Nina ari, ni shauku ya ushindi kwa mechi zote zilibaki.
Jina Kamili: Ally Hussein Msengi
Terehe ya Kuzaliwa: Desemba 20, 2001
Mkoa anakotoka: Mwanza
Nafasi Anayocheza: Beki wa Kati-Libero
Jezi Namba: 14
Maoni: Huu ndio wakati wetu, hakuna kulala, hakuna kurudi nyuma mpaka fainali za Kombe la Dunia.
Jina Kamili: Issa Abdi Makamba
Terehe ya Kuzaliwa: Aprili 13, 2001
Mkoa anakotoka: Dodoma
Nafasi Anayocheza: Beki wa Kati-Sentahafu
Jezi Namba: 6
Maoni: Tumetoka mbali, hatuwezi kuwaangusha Watanzania.
Jina Kamili: Kelvin Nashon Naftal
Terehe ya Kuzaliwa: Agosti 2, 2000
Mkoa anakotoka: Dar es Salaam
Nafasi Anayocheza: Kiungo wa kushambulia
Jezi Namba: 7
Maoni: Kila mechi fainali mpaka Madagascar tena na Kombe la Dunia.
Jina Kamili: Ally Hamisi Ng’anzi
Terehe ya Kuzaliwa: Septemba 3, 2000
Mkoa anakotoka: Mwanza
Nafasi Anayocheza: Kiungo Mkabaji
Jezi Namba: 2
Maoni: Mpaka hapa tulipofika, hakuna kushindwa tena. Tunaomba dua kwa Watanzania.
Jina Kamili: Asadi Ali Juma
Terehe ya Kuzaliwa: Aprili 15, 2001
Mkoa anakotoka: Unguja, Zanzibar
Nafasi Anayocheza: Kiungo Mshambuliaji
Jezi Namba: 10
Maoni: Pamoja tutashinda.
Jina Kamili: Enrick Vitalis Nkosi
Terehe ya Kuzaliwa: Januari 15, 2000
Mkoa anakotoka: Dar es Salaam
Nafasi Anayocheza: Beki wa Kati-Libero
Jezi Namba: 4
Maoni: Sina shaka na wenzangu, tuko safi na ninaamini tutashinda.
Jina Kamili: Ibrahim Abdallah Ali
Terehe ya Kuzaliwa: Septemba 8, 2000
Mkoa anakotoka: Unguja, Zanzibar
Nafasi Anayocheza: Mshambuliaji
Jezi Namba: 17
Maoni: Akili yangu ni kuwapa faraja Watanzania kwa kuwapa ushindi.
Jina Kamili: Mohammed Abdallah Rashid
Terehe ya Kuzaliwa: Juni 12, 2000
Mkoa anakotoka: Dar es Salaam
Nafasi Anayocheza: Kiungo Mshambuliaji
Jezi Namba: 11
Maoni: Lengo letu ni kufanikiwa kama timu na ndipo taifa litakapojua kuwa tumeshamiria.
Jina Kamili: Yohana Oscar Mkomola
Terehe ya Kuzaliwa: Aprili 18, 2000
Mkoa anakotoka: Dar es Salaam
Nafasi Anayocheza: Mshambuliaji
Jezi Namba: 15
Maoni: Hii ni vita, hakujashusha silaha hadi turudi Madagascar 2017.
Jina Kamili: Muhsin Malima Makame
Terehe ya Kuzaliwa: Desemba 10, 2000
Mkoa anakotoka: Pwani
Nafasi Anayocheza: Mshambuliaji
Jezi Namba: 19
Maoni: Hapa Kazi tu, mpaka kieleweke.
Jina Kamili: Shaban Zuberi Ada
Terehe ya Kuzaliwa: Novemba 24, 2001
Mkoa anakotoka: Dar es Salaam
Nafasi Anayocheza: Kiungo Mkabaji
Jezi Namba: 13
Maoni: Hakipiti kitu kwangu, nyuma nakaba mbele nashambulia.
Jina Kamili: Syprian Benidictor Mtegesigwa
Terehe ya Kuzaliwa: Juni 6, 2000
Mkoa anakotoka: Mwanza
Nafasi Anayocheza: Kiungo Mshambuliaji
Jezi Namba: 8
Maoni: Ushindi ni lazima kwa kila mechi.
No comments:
Post a Comment