Utumiaji wa zana bora za kiasasa za kilimo kama hizi utakuwa ni ndoto
ikiwa tutaendeleza siasa badala ya kuangalia shughuli za maendeleo na
kutatua changamoto mbalimbali.
Na Daniel Mbega
NI miezi
tisa sasa tangu serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani. Na iliingia
katika kipindi ambacho Watanzania walikuwa wanaimba wimbo mmoja tu
‘MABADILIKO’.
Wananchi
walikuwa wamechoshwa na umaskini, ukosefu wa huduma za msingi za kijamii kama
afya, elimu, maji safi, miundombinu na kadhalika, ambazo zilikuwa ni kilio chao
cha miaka mingi bila kupatiwa ufumbuzi.
Kikubwa
kilichokuwa kinapigiwa kelele na wananchi ni kero ya rushwa na ufisadi, uzembe,
ubadhirifu wa mali ya umma na mambo mengine ambayo kwa kiasi kikubwa
yamekwamisha maendeleo kwa kipindi kirefu.
SOMA ZAIDI
SOMA ZAIDI
No comments:
Post a Comment