Mganga Mku wa Mkoa wa Tanga (RMO)
Dkt Asha Mahita akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mbunge wa Jimbo
la Tanga (CUF) ambaye alikwenda kuitembelea hospitali ya Mkoa wa Tanga
Bombo kuangalia changamoto zinazowakabili.
Mbunge wa Jimbo la Tanga
(CUF) Mussa Mbaruku akisisitiza jambo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga
(RMO) Dkt Asha Mahita
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF)
Mussa Mbaruku katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari kutoka
katika taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Sunshine Muslim
Volunteer huku wakishirikiana na madaktari bingwa kutoka nchi za
Uingereza,
Afrika kusini, Canada na Pakistani waliokuja kuweka kambi ya siku tano
kwa
ajili ya kutoa matibabu bure ya Fistula.
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF),
Mussa Mbaruku ameombwa kuangalia namna ya
kuweka mkakati wa kuvisaidia vituo vya afya na Zahanati zilivyopo ndani ya Jiji
la Tanga ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya mkoa wa Tanga
Bombo inayohudumia wagonjwa wa mkoa mzima.
Ombi hilo lilitolewa jana na
Mganga Mku wa Mkoa wa Tanga (RMO) Asha Mahita
wakati Mbunge huyo alipoitembelea hospitali ya alisema kuwa msongamano
unaoikabili Hospitali ya Rufaa ya Mkoa unatokana na kutokuwepo na ubora katika
zahanati na vituo vya afya jambo ambalo linalowafanya wanachi kukimbilia katika
Hosptiali hiyo.
Hatua hiyo inatokana na
zahanati na vituo vya afya vingi Jijini Tanga kukakabiliwa
na changamito nyingi zinazo sababisha kukosa ubora hali inayochangia kwa
asilimia kubwa wananchi wengi kukimbilia katika hospital ya Rufaa ya Bombo na
kuongeza msongamano wa wagonjwa.
Mahita alisema ipo haja ya
kuvisaidia vituo hivyo ambavyo havina nyumba za
watumishi, uzio, miundombinu mibovu na vingine kukosa umeme jambo ambalo
linakuwa si rafiki kwa wahudumu na linakwamisha shughuli za kiafya hasa nyakati
za usiku.
Alisema kuwa iwapo kutakuwepo
na mabororesho katika vituo hivyo huku Serikali
na wadau mbalimbali wakiweka nguvu zao katika swala la kumalizia
Hospitali ya wilaya
ambayo mpaka sasa inajengo moja la ghorofa kwa ajili ya utawala ikimaliziwa na
kuanza kutumika kutapunguza kwa asilimia kubwa msongamano kwenye
hospitali hiyo.
Kwa upande wake, Mbunge Mussa
Mbaruku alihaidia kuangalia namna ya kuzipatia
ufumbuzi changamoto hizo kwani wananchi afya zao zinapokuwa zimeimarika
inawasaidia kuweza kufanya shughuli za kujiingizia kipato.
“Ndugu zangu huu si muda wa
kupiga porojo kuhusiana na masuala ya afya
ambalo ndio uti wa mgongo wa wananchi hivyo lazima viongozi
wajenge umoja na kutafuta njia
ya kuweza kuviboresha vituo hivyo ambavyo vitawasaidia kwa asilimia kubwa
wananchi kupata huduma hiyo kwa ukaribu zaidi “Alisema
Aidha alisema pamoja na
changamoto zinazozikabili zahanati na vituo hivyo
lazima Serikali itenge fedha za kutosha ili kuweza kuimalizia Hospitali ya
Wilaya iliyopo Masiwani Shamba ambayo mpaka sasa bado hakuna majibu sahihi ya
kukwama kwa umaliziwaji wa Hosptili hiyo.
“Bado nashindwa kupa majibu ni
kitu gani kinachokwamisha kumalizika kwa
Hospitali ya Wilaya ambayo tayari inajengo zuri la utawala tena la ghorofa
serikali inawajibu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha Hospitali
hiyo inamalizika na inakuwa na kiwango bora katika sekta zote za
matibabu.
Mbaruku alifanya mazungumzo
hayo na mganga mkuu wa Mkoa alipo watembelea
madaktari kutoka katika taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Sunshine Muslim
Volunteer huku wakishirikiana na madaktari bingwa kutoka nchi za Uingereza,
Afrika kusini, Canada na Pakistani waliokuja kuweka kambi ya siku tano kwa
ajili ya kutoa matibabu bure ya Fistula.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
No comments:
Post a Comment