By LEAH MUSHI
Chama
cha watanzania waliosoma China- China Allumni Association of Tanzania
(CAAT) hii leo tarehe 27 August, 2016 kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu
kwa ajili ya kupata viongozi wake wapya.
Uchaguzi
huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Rombo Green Views Hotel
Sinza jijini Dar es Salaam kuanzia saa saba kamili mchana na kufuatiwa
na sherehe ya kuwapongeza viongozi wapya na kuwaaga viongozi waliomaliza
muda wao.
Kwa
mujibu wa mwenyekiti wa uchaguzi wa chama hicho Gustav Sanga uchaguzi
huo utawaweka madarakani viongozi hao miaka mitatu kwa mujibu wa katiba
ya chama hicho.
Nafasi
zinazogombewa katika uchaguzi huo ni Mwenyekiti, Katibu, Mhazini,
Mkurugenzi wa Takwimu, Habari, Mkurugenzi wa Sanaa, Utamaduni na Urithi
pamoja na Mkurugenzi wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Sanga
pia amewakaribisha watanzania wote waliomaliza China kujiunga katika
chama hicho ili kuweza kutimiza malengo mbalimbali waliyojiwekea ikiwemo
kuishauri serikali masuala yahusuyo Tanzania - China.
Chama
hicho cha watanzania waliosoma China kina miaka sita tangu kuanzishwa
kwake na kina wanachama tangu waliosoma china miaka ya1980 kwa ngazi ya
shahada , astashahada na shahada ya uzamivu.
No comments:
Post a Comment