Wajumbe
wa Kamati ya Maendeleo kwa Afrika katika Bnge la Korea Kusini
wakiwasili katika uwanja mdogo wa ndege uliopo katika Hifadhi ya Taifa
ya Serengeti.
Meneja
Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA,Victor Ketance akipokea
ugeni wa wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha
kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema akipokea ugeni wa
wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha kisasa
cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema
akisalimiana na wadau wa utalii,Zainabu Ansel ,Mkurugenzi wa kampuni ya
Utalii ya Zara(katikati) na Mkurugenzi wa Kibo Safari's Willy
Chamburo.(kushoto) waliokuwepo uwanjani hapo.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Kibo Safari's ,Willy Chamburo (katikati) akizungumza
jambo na kiongozi wa ugeni wa Korea Kusini Won Yul Chui (kushoto) baada
ya kukutana katika uwanja mdogo wa ndege uliopo Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti .kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
William Mwakilema.
Wajumbe
wa Kamati ya Maendeleo ya Afrika katika Bunge la Korea Kusini wakitia
saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kuangalia eneo lililotengwa kwa ajili ya
ujenzi wa kituo cha kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema (kushoto)
akizungumza na Wajumbe wa kamati ya Maendeleoo ya Afrika ya Bunge la
Korea Kusini waliofika katika Hifadhi hiyo kwa ajili ya ufuatiliaji wa
maenedeleo ya kuanza kwa mradi wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha Taarifa
katika Hifadhi hiyo.
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,William Mwakilema akiongoza
Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini walioko katika kamati ya
Maendeleo ya Afrika kutembelea maeneo kutakapo jengwa kituo cha kisasa
cha taarifa.
Moja
ya eneo lilipo sasa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo
inatumika kutoa taarifa kwa njia ya picha za video za Hifadhi hiyo.
Ujumbe
wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakitizama picha ya Hayati Baba wa
Taifa ,Mwl Julius K. Nyerere akiwa na rafiki yake Prof,Dkt Bernhard
Grzimek huku wakipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema.
Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakipata maelezo katika
michoro ya kituo cha kisasa cha taarifa katika Hifadhi ya taifa ya
Serengeti.
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema akitoa zawadi
kwa wajumbe wa Bunge la Korea Kusini mara baada ya kutembelea eneo
kutakapo jengwa kituo cha kisasa cha taarifa katika hifadhi hiyo.
Wajumbe
wa Bunge la Korea Kusini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi na watumishi wa Shirika la Hifadhhi za Taifa (TANAPA ) na
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Na
Dixon Busagaga wa Michuzi blog Kanda ya Kaskazini.
Kituo hicho kinachotarajiwa kugharimu zaidi shilingi bilioni nne kitajengwa katika Hifahi ya Taifa ya Serengeti .
Tayari serikali ya Korea Kusini imeshatuma wajumbe wake kuja nchini tanzania kujionea eneo kitakapojengwa kituo hicho na kukamilisha taratibu nyingine muhimu ambapo kiongozi wa wajumbe hao Park Joosung amesema mradi huo ni mwendelezo wa ushirikiano wa Korea Kusini na Tanzania katika kuimarisha uhifadhi.
Akizungumza na ujumbe huo mkuu wa hifadhi ya taifa ya serengeti Wiliam Mwakilema amesema kituo hicho kikikamilika kitaongeza chachu utalii na kitatoa fursa kwa wageni kuona aina nyingi zaidi za wanyama.
Naye mratibu wa ujenzi bw Victor Ketance amesema ujenzi utaanza mwezi october mwaka huu na unatarajiwa kumalizika baada ya miezi 14.
No comments:
Post a Comment