Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akizindua rasmi Operesheni Ukuta jijini Dar es Salaam.
Na Daniel Mbega
FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), amekunjua makucha yake na kuuonyesha udikteta wake hadharani.
Amekwishatoa tamko kwamba, viongozi wa ngazi mbalimbali wa
chama hicho ambao watashindwa kuandaa maandamano ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania
(Ukuta), Septemba Mosi, mwaka huu, watakuwa wamepoteza sifa za kuwa viongozi,
kwani watakuwa
wamewasaliti wananchi ambao waliwachagua.
Chadema
imeitisha maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima kuanzia Septemba Mosi,
lakini Rais John Magufuli alionya akiwa ziarani Kanda ya Kati hivi karibuni
kuwa kutekeleza azma hiyo ni kumjaribu, na "kawaambie... sijaribiwi na sitakaa
nijaribiwe."
No comments:
Post a Comment