Hujafa
hujaumbika! Erasto Mketo (26) ni mkazi wa Lindi kijiji cha Mtondo Kimwaga, ni
mlemavu wa miguu na mikono ambaye ana ndoto nyingi za kujikwamua kimaisha kama
kijana mwingine wa Kitanzania, lakini ulemavu wake umekuwa changamoto kubwa ya
yeye kuweza kufanikisha ndoto zake.
Moja ya
changamoto zinazomkuta Erasto ni pamoja na unyanyapaa hasa kwenye sekta ya
ajira jambo lililomfanya apaze sauti na kuwaomba Watanzania wajitokeze
kumsaidia hata kwa kumpa mtaji au ajira ili aweze kujikwamua kimaisha.
Akiongea na
mwandishi wa Blogs za Mikoa Tanzania, Erasto alisema anaamini anaweza kufanya biashara
yoyote kama muajiriwa au kama atapewa mtaji wa kufungua biashara yake mwenyewe.
“Kwa huku
kijijini nimekuwa nikipata tabu sana ya kupata ajira ambayo itaendana na
ulemavu wangu na elimu yangu ya shule ya msingi, lakini ningependa sana
nitimize ndoto zangu kwa sababu naweza sana kufanya biashara.
“Nawaomba
watanzania wenzangu mnisaidie hata kwa kuniajiri ili mradi na mimi nijikwamue
kiuchumi kama wenzangu na hata niweze kuwasaidia wazazi wangu,” alisema Erasto
huku akiongeza kuwa baiskeli ya kutembelea atainunua mwenyewe kupitia ajira
yake ikiwa atapata mtu wa kumuajiri.
Kutoa ni moyo
si utajiri, kama umeguswa tafadhali msaidie Mtanzania mwenzako kwa hali na mali
kupitia namba 0682755874, imesajiliwa kwa jina la Anastansi Ngomba.
No comments:
Post a Comment