Mchezaji wa Simba Fredrick Magnon akiruka juu na golikipa wa
Ndanda FC Jackson Chove huku wachezaji wa timu hiyo wakiangalia wakati mchezo
huo wa Ligi Kuu ukiendelea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Jumamosi, Agosti 20, 2016. Simba ilishinda 3-1.
SIMBA SC imeanza kwa kuongoza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara kufuatia ushindi wake mkubwa wa mabao 3-1 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara katika
mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi, Agosti 20, 2016.
Kasi ya mchezo huo ilikuwa nzuri kwa Simba, ambayo mashabiki
wa timu hiyo wanahoji iwapo itaendelea hivyo hivyo na kurejea kwenye ufalme
wake au itakuwa kama moto wa mabua unaozima punde.
No comments:
Post a Comment