Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba(kushoto), akimsikiliza Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu
Youqing (katikati), wakati wa mazungumzo juu ya masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi
na usalama kati ya Tanzania na China,
Kulia ni Msaidizi wa Balozi, Wang Fang. Mazungumzo hayo yalifanyika leo,jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba(katikati), akiangalia vipengele mbalimbali vinavyohusu
ushirikiano juu ya masuala ya ulinzi na usalama, wakati wa mazungumzo
yaliyomhusisha Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing(kulia). Kushoto
ni Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong. Mazungumzo hayo
yalifanyika leo,jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa
China, Lin Zhiyong(kulia), Msaidizi wa Balozi wa China nchini Tanzania, AI
Zhuan(katikati) na Katibu wa Balozi, Dong Zhenyu(kushoto), wakimsikiliza Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(hayupo pichani), wakati wa
mazungumzo juu ya masuala ya ushirikiano
katika sekta ya ulinzi na usalama kati
ya Tanzania na China. Mazungumzo hayo yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba(katikati), akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa
China, Lin Zhiyong, mara baada ya kumaliza mazungumzo juu ya masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi
na usalama kati ya Tanzania na China. Kulia
ni Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing. Mazungumzo hayo
yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba(kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China
nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing, mara baada ya kumaliza mazungumzo juu ya masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi
na usalama kati ya Tanzania na China. Mazungumzo
hayo yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO
SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment